Home Azam FC FEISAL SALUM LEO MKWAWANI KUNACHIMBIKA , YANGA WAJIPANGE

FEISAL SALUM LEO MKWAWANI KUNACHIMBIKA , YANGA WAJIPANGE

Fei toto Azam FC leo

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ameonekana kuwa mwenye tabasamu muda wote akiwa Mkwakwani jijini Tanga.

“Angalia nyuso za furaha kwenye mazoezi ya mwisho leo (jana) Jumanne jioni kabla ya kuivaa Yanga,” Azam FC

Fei Toto aliyetokea Young Africans Sports msimu uliyopita atawakabili waajiri wake wa zamani Yanga SC kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Ngao ya Jamii leo Jumatano saa 1:00 usiku.

Zanzibar finest ni usajili mpya wa Azam FC uliyobeba matumaini makubwa ya kuwafikisha kwenye Nchi ya ahadi.

Mara ya mwisho Azam kukutana na Yanga katika Uwanja wa Mkwakwani alikubali kipigo cha goli 1-0 kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la FA.

SOMA NA HII  PROFESA JAY ATEMBELEWA NA KIONGOZI WA SIMBA