Home Yanga SC JEMBE LA KAZI LAVUTWA NA KAZE,KUIVAA MBEYA CITY

JEMBE LA KAZI LAVUTWA NA KAZE,KUIVAA MBEYA CITY


 BAKARI Mwamnyeto,nahodha msaidizi wa kikosi cha Yanga amerejea kambini baada ya kuwa na ruhusa maalumu kutokana na matatizo ya kifamilia.

Mwamnyeto ambaye amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Lamine Moro ambaye ni nahodha safu yao ya ulinzi ni namba moja kwa kuruhusu mabao machache.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 imeruhusu mabao 7 huku watani zao wa jadi, Simba wakiwa wameokota jumla ya mabao 8 baada ya kucheza mechi 17 ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.
Chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze amekuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza na ana bao moja pia kibindoni kati ya 29 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44.
Hakuwa sehemu ya kikosi kilichomenyana na African Sports ya Tanga kwenye mchezo wa kirafiki ambapo timu hiyo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Mchezo wao wa ligi unaofuata ni dhidi ya Mbeya City unaoatarajiwa kuchezwa Februari 13, Uwanja wa Sokoine Mbeya na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho.
SOMA NA HII  MAZEMBE KUMSAJILI NABI...USAJILI YANGA GSM AFANYA KUFURU CONGO