Home news JINSI YANGA WALIVYOUTEKA MSIBA WA SONSO JANA…MANARA,NABI NA WAZUA TAFRANI…MAYELE AGOMA …

JINSI YANGA WALIVYOUTEKA MSIBA WA SONSO JANA…MANARA,NABI NA WAZUA TAFRANI…MAYELE AGOMA …


KIKOSI cha Yanga kimezusha vurugu mbalimbali katika mazishi ya beki wao wa zamani Ally Mtoni ‘Sonso’ huku mshambuliaji Fiston Mayele na kocha wake Nesreddine Nabi wakiwateka waombolezaji.

Yanga ambao walifika wakati mwili wa Sonso ukifika makaburini walipofika waliwalazimisha walinzi wao maarufu kama makomandoo kufanya kazi ya ziada kuwatuliza watu ambao walianza kuwakimbilia wachezaji wao.

Waombolezaji hao walianza kumshangilia kocha wa Yanga Nabi mara baada ya kufika makaburini hapo huku Mayele akianza kusakwa.

Walipomuona Mayele vurugu za kutaka kupiga picha na mshambuliaji huyo zilizidi huku baadhi wakitaka awaonyeshe tena mtindo wake wa kushangilia anapofunga bao.

Hata hivyo mshambuliaji huyo aligoma huku akiwoamba radhi mashabiki hao kisha wakaendelea nba taratibu za mazishi.

Hata hivyo mara baada ya kumaliza mazishi kikosi cha Yanga kilikwenda mpaka nyumbani kwa wazazi wa Sonso kutoa mkono wa pole ambapo magari yalilazimika kusimama upande mmoja kupisha basi la Yanga kupita vizuri sambamba na masafara wa watu ambao walikuwa wakilisindikiza.

Hapo nyumani nako waombolezaji mbalimbali walionekana kupambana kupiga picha timu hiyo huku kila mtu akimsaka mchezaji anayetaka kumuona ampige picha.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAKEKE YA OKRAH....KOCHA MAKI KAGUNA ..KISHA AKASEMA HAYA...ATIA 'NDIMU' USAJILI MASTAA WAPYA...