Home news KISA MAYELE…NABI ABUBUJIKWA MANENO HAYA…MAKAMBO , YUSUPH NA NGUSI WAJIPANGE….

KISA MAYELE…NABI ABUBUJIKWA MANENO HAYA…MAKAMBO , YUSUPH NA NGUSI WAJIPANGE….


KOCHA wa Yanga, Nesreddine Nabi amechekelea msako wa mabao kwa kikosi chake katika mechi walizocheza hadi sasa, lakini akampa tano zaidi straika namba moja wa kikosi hicho, Fiston Mayele akisema jamaa anajua sana kusumbua.

Nabi alisema anavutiwa na Mayele jinsi anavyoongoza jahazi la kusaka mabao bila kujali kuna wakati yanakataliwa.

Mayele aliyesajiliwa msimu huu kutoka DR Congo, ameifunga Yanga mabao sita katika Ligi Kuu Bara na mawili ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kuifanya timu hiyo itishe.

Yanga inalisotea taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo sasa huku kwa ASFC inalisaka kwa msimu wa tano, kwani ilibeba mara ya mwisho ule wa 2015-2016.

Nabi alisema baada ya kukataliwa kwa bao lake la kwanza katika mchezo wa juzi dhidi ya Biashara United wa hatua ya 16 Bora ya ASFC, mshambuliaji huyo hakukata tamaa badala yake alipambana kuisaidia Yanga kushinda mabao 2-1.

Mayele alifunga bao la pili baada ya Yannick Bangala kufungua pazia na Biashara ikapata la kufutia machozi kupitia Collins Opare aliyemalizia pasi ya Christian Zigah na kuivusha Yanga hadi robo fainali.

Katika mchezo wa juzi wakati Yanga ikicheza dhidi ya Biashara, Mayele alifunga bao dakika ya pili, lakini lilikataliwa kwa sheria ya mtego wa kuotea ambapo baada ya picha za marejeo zilionyesha ni kweli ilikuwa usahihi kukataliwa kwa bao hilo.

“Mchezaji mwenye moyo mwepesi baada ya kukataliwa kwa lile bao angeweza kutoka mchezoni na kukata tamaa kwa mambo ambayo pia yalitokea hapa kati, lakini kwake (Mayele) haikuwa hivyo,” alisema Nabi.

“Angalia alivyoendelea kupambana kwa nguvu na kasi kubwa kusaka ushindi zaidi. Ni mpambanaji sana hakati tamaa wala haogopi mabeki hata wakimuumiza.”

Vilevile Nabi alifichua kwa-mba aliwa-ambia ma-staa wa-ke kwa-mba katika kukabiliana na makosa ya waamuzi kukata mabao yao wanachotakiwa ni kufunga zaidi kwa kuwa hayawezi kukataliwa mabao yote.

Alisema mashabiki wa timu yao bado wanatarajia kuona kikosi chao kikipambana bila kujali changamoto ambazo wanapitia na kwamba ili malengo yao yatimie wanatakiwa kufunga mabao zaidi yatakyowahakikishia ushindi.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIWAZA UBINGWA KWANZA..NABI WALA HAFIKIRI HILO KUMBE...HIKI HAPA KIPAUMBELE CHAKE..

“Kuna makosa kidogo kila mtu anayaona lakini sio kila wakati utatakiwa kulalamika unatakiwa kuendelea kupambana niliwaambia tunatakiwa kufunga zaidi kutumia nafasi nyingi tunazotengeneza.

“Mfano unaweza kuangalia mchezo dhidi ya Mbeya City hatukutakiwa kupata pointi moja, lakini tulitakiwa kutumia nafasi zaidi kuliko ile ambayo tutaendelea kuikumbuka.

“Sasa wachezaji wameanza kuelewa na ndio maana unaona kila mmoja anapambana anataka kuona ushindi unapatikana kama ni beki akipata nafasi anataka kuitumia kwa ushindi ni wetu sote.”