Home news WAKATI YANGA WAKIWAZA UBINGWA KWANZA..NABI WALA HAFIKIRI HILO KUMBE…HIKI HAPA KIPAUMBELE CHAKE..

WAKATI YANGA WAKIWAZA UBINGWA KWANZA..NABI WALA HAFIKIRI HILO KUMBE…HIKI HAPA KIPAUMBELE CHAKE..


ACHANA na mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi, amewaambia wachezaji wake anataka kuona mambo mawili yakifanyika katika kila mchezo watakaoucheza.

Hiyo ni baada ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 45, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Simba SC wenye 34 kabla ya jana kucheza dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Msimu huu Yanga imepania kuivua ubingwa Simba baada ya kuukosa kwa misimu minne ambapo mara zote Simba wametawala.

Nabi alisema jambo la kwanza ambalo analitaka likifanywa na wachezaji wake ni kucheza soka safi la kuvutia lenye mchanganyiko wa pasi nyingi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki.

Nabi alisema jambo la pili ni timu kupata ushindi mnono katika kila mchezo uwe wa ligi au Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Aliongeza kuwa, anaamini wachezaji wake watafuata maagizo yake na kufanikisha hayo yote, licha ya kikosi chake kuandamwa na majeruhi wengi.

“Lipo wazi ligi ni ngumu, lakini hiyo isitufanye kupoteza malengo yetu tuliyojiwekea msimu huu ambayo ni kubeba makombe yote.

“Lengo langu la kwanza katika timu kuona inacheza soka safi, lingine kupata ushindi na siyo kujilinda, katika hilo nashukuru nimeanza kuliona.

“Mfano mchezo wetu wa ligi dhidi ya Geita, tulicheza soka safi la kutojilinda ambalo liliwavuruga wapinzani wetu na kufanikiwa kupata matokeo mazuri.

“Tuliwaheshimu Geita lakini sio kwamba wametuzidi baada ya kucheza katika kiwango bora, ubora wao umetokana na sisi kikosi chetu kuwa na majeruhi wengi ambao hivi karibuni wataanza kuonekana baada ya kupata nafuu baadhi yao.

“Kila siku ninaendelea kuwaongezea mbinu wachezaji wangu zitakazotufanya tuendelee kuwa bora na kucheza katika kiwango kizuri zaidi ya sasa wanachokionesha,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  HUKO SIMBA NAKO PA MOTO BALAAH....MASHINE HII YA MAGOLI KUTOKA COLOMBIA KUTUA TZ MUDA WOWOTE..