Home news KISA UKAME WA MAGOLI…MUGALU AMWAGA CHOZI…ADAI HUU NI MWISHO WAKE KUCHEZA MECHI…

KISA UKAME WA MAGOLI…MUGALU AMWAGA CHOZI…ADAI HUU NI MWISHO WAKE KUCHEZA MECHI…


CHRIS Mugalu alimaliza msimu uliopita na mabao 15 akishika nafasi ya pili ya wafungaji bora nyuma ya John Bocco, lakini msimu huu straika huyo mambo yamekuwa magumu kwake na kukiri kuwa anapitia kipindi kigumu.

Mugalu alisema katika maisha yake ya soka la ushindani hajawahi kupitia kipindi kigumu kama wakati huu ndani ya Simba.

“Kuna wakati huwa nashindwa kufunga, ila haijawahi kuwa kipindi kirefu kama hiki nilichonacho Simba, kwani mara nyingi hata nikitoka majeruhi nikirudi naendelea na ukali wangu wa kufunga mabao,” alisema Mugalu.

Straika huyo alisema kwa sasa analichukulia changamoto anayopotia kama darasa la kujifua zaidi ili arejeshe makali yake binafsi kwa faida ya timu ya Simba.

“Binafsi naimani kubwa mno huu ni mwisho kwangu kucheza mechi nyingi bila kufunga nimefanya mazoezi yangu binafsi pamoja na kujiandaa vya kutosha kusikiliza yale ya benchi la ufundi ili kwenda kutimiza yale ambayo kila mmoja anatamani kuona kutoka kwangu,” alisema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  MAPYA YAIBUKA MSOTO WA BENCHI KWA MAKAMBO...NABI ASHINDWA KUVUMILIA..AANIKA YOTE...