news

KISA YANGA KUSHINDWA KUPATA USHINDI JUZI…SERIKALI YAPANGA KULETA VAR KWENYE LIGI YA BONGO…

admin February 7, 2022 10:27 am


BAADA ya matukio mengi ya soka kwa upande wa waamuzi kutokufuata sheria 17 Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ameibuka na kutaja suruhu.

Nchemba ameibua hayo baada ya jana Yanga kunyimwa nafasi ya wazi ya kufunga bao kwa mwamuzi msaidizi kuashiria ameotea (offside).

Kupitia mtandao wake wa kijamii Instagram Nchemba amependekeza kuweka chombo kitakacho msaidia mwamuzi kurudia tukio uwanjani (VAR).

“Nitaongea na Waziri mwenzangu anayesimamia michezo bajeti ijayo tumtafutie fedha, tuweke VAR viwanja hata 10 ambayo itasaidia kupunguza makosa yaliyopo,” anaandika na kuongeza;

“Pia tuweke nyasi bandia kuondoa utaratibu wa kucheza mpira shambani, haya ndio maeneo yanayolalamikiwa sana kwenye ligi yetu,” alisema na kuongeza kuwa Yanga jana kama sio makandokando ya waamuzi ilistahili kushinda.

WAKATI CHAMA AKIIRUDISHA SIMBA KWENYE SAYARI YAKE…BOCCO MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU..UKWELI UKO HIVI.. WAKATI SIMBA WAKINYATIA SAINI ZA KINA MWAMNYETO…YANGA WAIBUKA NA KUTOA KAULI HII..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply