Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…MTIBWA SUGAR WARUSHA DONGO JINGINE YANGA…WATAMBA KUTIBUA REKODI YAO…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…MTIBWA SUGAR WARUSHA DONGO JINGINE YANGA…WATAMBA KUTIBUA REKODI YAO…


Mabingwa wa Tanzania Bara msimu wa 1998/99 na 1999/2000 Mtibwa Sugar, wametoa tahadhari kubwa kwa Vinara wa sasa wa Ligi Kuu Young Africans, kuelekea mchezo wa Mzunguuko 15.

Mtibwa Sugar itakua mweneyji wa mchezo huo, kesho Jumatano (Februari 23), Uwanja wa Manungu Complex, huku ikitangaza dhamira ya kubakisha alama tatu muhimu nyumbani kwao mkoani Morogoro.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kikosi chao kipo tayari kuvunja rekodi ya Young African ya kutopoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kifaru, amesema wanafahamu kuwa mchezo dhidi ya Young Africans utakuwa wa mwisho kumaliza mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, hivyo kutokana na nafasi mbaya waliyopo kwenye msimamo, lazima wahakikishe wanapata ushindi.

“Kikosi kinaendelea kunolewa na Kocha Mkuu Salum Mayanga, nafahamu kuwa Kocha Mayanga ana kazi kubwa sana ya kufanya mazoezini kuelekea mchezo huu kutokana na kupoteza michezo miwili iliyopita.

“Licha ya hivyo, lakini morali ya wachezaji ni kubwa, wanafahamu umuhimu wa mchezo huu, hivyo najua watafuata maelekezo muhimu ya mwalimu na watafanikiwa kuyatimiza.

“Mechi hii itakuwa moja ya mechi kubwa ya mzunguko wa kwanza kwenye ligi kwa sababu Young Africans watahitaji kuendeleza rekodi ya ya kutopoteza, wakati Mtibwa tukihitaji alama tatu kujinasua kwenye nafasi mbaya tuliyopo.

“Tunafahamu Young Africans haijafanikiwa kupoteza mchezo wowote wa ligi kuu tangu kuanza kwa msimu huu, lakini hilo halitutishi, tutahakikisha tunawaonjesha utamu wa pilipili uwanjani, tutawaonesha maana halishi ya ushindani, nawaambia tukutane Februari 23,” amesema Kifaru.

Ikumbukwe kuwa, Mtibwa Sugar itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC kwa mabao 3-1 pamoja na kutolewa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Coastal Union kwa kipigo cha 2-0 mbele ya Coastal Union Jijini Tanga.

SOMA NA HII  MERIDIAN BET INAKUREJEAHEA 15% UKICHEZA VIRTUAL