Home news KUELEKEA MECHI YAO NA YANGA..MTIBWA WAMUIBUA UPYA DEO KANDA…KIFARU AWEKA WAZI KILA...

KUELEKEA MECHI YAO NA YANGA..MTIBWA WAMUIBUA UPYA DEO KANDA…KIFARU AWEKA WAZI KILA KITU…


MTIBWA Sugar imethibitisha kuwa muda wowote kuanzia sasa, itaanza kumtumia winga wao raia wa DR Congo, Deo Kanda baada ya kila kitu kukamilika.

Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, amesema kuwa walikuwa wanashindwa kumtumia nyota huyo kwa sababu kuna vitu kuhusu uhamisho wake vilikuwa havijakamilika ila kwa sasa kila kitu kipo sawa.

Akizungumza na gazeti la  Championi Ijumaa,   Kifaru alisema: “Tunatarajia kuanza kumtumia Deo Kanda hivi karibuni changamoto ilikuwa upande wa wenzetu kushindwa kutuma kibali chake.

“Deo Kanda tulimsajili sisi wakati wa dirisha dogo ila hakuwa anaonekana uwanjani kwa sababu ya kibali chake lakini mawasiliano yamefanyika tayari na wenzetu.

“Na tutakipata hivi karibuni, yeye mwenyewe anatamani kuitumikia Mtibwa Sukari. Kama itakuwa sawa huenda akacheza dhidi ya Yanga.”

Kanda aliibuliwa na Motema Pemba ya DR Congo, kisha akajiunga na TP Mazembe, Vita Club, Raja Raja Casablanca, Simba na nyingine.

SOMA NA HII  CHEZA SLOTI YA EUROPEAN ROULETTE UPATE HELA KUPITIA MERIDIANBET CASINO...