Home news SIMBA WAINGIA NIGER NA KIBURI CHA GOLI 10…MANGUNGU AVIMBA KICHWA…WANIGER WAWACHABO TU…

SIMBA WAINGIA NIGER NA KIBURI CHA GOLI 10…MANGUNGU AVIMBA KICHWA…WANIGER WAWACHABO TU…


KUELEKEA michezo yao miwili ya ugenini ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa umekamilisha maandalizi yote muhimu ya michezo hiyo, huku wakitamba kuwa wanataka kuvuna pointi zote sita za ugenini.

Simba inakwenda kwenye michezo hiyo ikiwa imeweka rekodi ya kufunga mabao 10 katika michezo miwili iliyopita jijini Dar es Salaam – ushindi wa 3-1 dhidi ya Asec Mimosas kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, na ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Kiwango walichokionyesha kwenye mechi hizo mbili, kimetosha kuwaaminisha mashabiki wao kuwa Simba imerejea kwenye makali yake, na sasa wanaamini kikosi chao hakikamatiki.

Simba ambayo imepangwa kundi D la michuano ya kimataifa ya Shirikisho, inatarajiwa  kuvaana na USGNkeshokutwa Jumapili nchini Niger, kabla ya kucheza dhidi ya RS Berkane nchini Morocco Februari 27.

Kuelekea michezo hiyo, tayari maafisa wa Simba wameshawasili nchini Niger kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya sehemu ambayo timu inayoondoka leo itafikia na kujifua kuelekea mchezo huo.

Akizungumza na gazeti la Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema: “Kwanza kama sehemu ya uongozi wa Simba napenda kuwapongeza wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa ujumla kwa ushindi mnono dhidi ya Ruvu Shooting.

“Ushindi huo umezidi kutupa ari ya kufanya vizuri kuelekea michezo yetu miwili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN na RS Berkane ambayo kama uongozi tumefanya maandalizi yote kuhakikisha tunapata pointi zote sita ugenini, kabla ya kurejea tena kujipanga kwa ajili ya michezo miwili ya nyumbani, tunaamini kutokana na maandalizi tuliyoyafanya tutafanikiwa.”

SOMA NA HII  KISA MKUDE....PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA ALIVYOMVURIGIA MIPANGO YAKE...