Home Habari za michezo KISA MKUDE….PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA ALIVYOMVURIGIA MIPANGO YAKE…

KISA MKUDE….PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA ALIVYOMVURIGIA MIPANGO YAKE…


PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao hawajawa fiti wanavuruga mipango ya timu hiyo kutokana na kumpa kazi ya kubadili kikosi cha ushindi.

Miongoni mwa wachezaji ambao hawajawa fiti kwa sasa ndani ya Simba ni pamoja na kiungo wa kazi Jonas Mkude na mshambuliaji Chris Mugalu.

Pablo alisema kila mchezaji ana umuhimu katika kikosi hicho, hivyo pale inapotokea mmoja kati yao akapata matatizo ni shida kwa timu nzima.

“Unaweza ukawa na wachezaji ambao wapo benchi, lakini hawapo fiti kutokana na kuwa wametoka kwenye majeraha, hilo linanifanya nipange kikosi upya.

“Ambacho ninakifanya ni kuona nao wanakuwa imara taratibu kwa kuwa hawawezi kuanza moja kwa moja kwenye ule ubora wao hasa ukizingatia kwa mechi zilizopo zote ni muhimu kwetu kushinda,” alisema Pablo.

SOMA NA HII  KUHUSU MBRAZILI SIMBA KUMKUBALI GHAFLA....MINZIRO AANIKA 'UCHAWI' ANAOTUMIA KIBU DENIS..