Home Habari za michezo DILI LA MWENDA KUJIUNGA SIMBA LAFIA NJIANI….ARUDI KWAKO KENYA KIMYA KIMYA…MABOSI WAGAWANYIKA…

DILI LA MWENDA KUJIUNGA SIMBA LAFIA NJIANI….ARUDI KWAKO KENYA KIMYA KIMYA…MABOSI WAGAWANYIKA…


WINGA wa Kabwe Warriors, Mkenya Harrison Mwendwa amerudi kwao Kenya bila kusaini Simba baada ya kutofikia muafaka huku ikielezwa kwamba uongozi umeamua kuachana na dili hilo kimyakimya baada ya kufanya tathmini ya kina.

Mwendwa aliwasili nchini wiki iliyopita kwa ajili ya kukamilisha dili lake na Simba iliyoonyesha nia ya kumuhitaji tangu dirisha dogo la usajili msimu huu.

Mwendwa alitarajiwa kukamilisha dili hilo na haraka kurudi kwao Jumapili ila mambo yalikuwa tofauti na vile ambavyo alitegemea mara baada ya kufika nchini huku akikumbana na kejeli kibao za mashabiki mitandaoni.

Iko hivi, Mwendwa akiwa sambamba na wakala wake walifanya mazungumzo na Simba kama walivyokubaliana awali hadi kumleta nchini ila hawakufikia muafaka na inaelezwa sababu kubwa ni mabosi wa timu hiyo kugawanyika kwani wengi wao hawajaridhishwa na kiwango chake kwasasa na hata muitikio wa mashabiki wa Simba kwenye mitandao ya kijamii.

Mwendwa alisema amerudi kwao kuendelea na mapumziko baada ya kushindwa kukubaliana na Simba kama alivyotegemewa awali.

Mwendwa anatajwa pia kufanya mazungumzo na Singida Big Stars ambao wamepanda daraja kucheza ligi kuu, hata hivyo alisema suala la usajili wake kwasasa anamuachia wakala wake. Ofisa Mtendaji mkuu wa Singida Big Boys, Muhibu Kanu alisema kwenye faili yake hawajamsajili Mwendwa.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE