Home Uncategorized NYOTA POLISI TANZANIA APATA MUDA WA KUWA KARIBU NA MKE WAKE

NYOTA POLISI TANZANIA APATA MUDA WA KUWA KARIBU NA MKE WAKE


SIXTUS Sabilo mtupiaji wa klabu ya Polisi Tanzania amesema kuwa kutokana na mapumziko ya lazima kwa wachezaji wa Ligi Kuu Bara Bongo yamemfanya amekuwa karibu na mke wake pamoja na familia kiujumla.
Kabla ya Ligi Kuu Bara kusimishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambalo ni janga la dunia Sabilo alikuwa kambini Moshi huku familia yake ikiwa Mara.
Sabilo amesema kuwa muda mwingi kwa sasa amekuwa na familia yake jambo ambalo awali ilikuwa ngumu kutokea kwake kutokana na kutumia muda mwingi kazini.
“Kutokana na janga la Virusi vya Corona kwa sasa nimetulia zangu nyumbani huku Bunda nikiwa na familia yangu jambo ambalo awali ilikuwa ngumu kufanya kutokana na ratiba kunibana.
“Ninapata muda wa kuwaelekeza watoto wangu ambao Mungu amenijalia kuwapata kwa sasa watatu na mke wangu pia tumekuwa tukipata wasaa wa kuzungumza mengi pamoja na kubadilishana mawazo, hivyo maombi yetu hili janga lipite turejee kwenye shughuli zetu kama zamani,” amesema, Sabilo ambaye ametupia mabao saba.
SOMA NA HII  MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI