Home BIashara United RASMI….AZAM FC WAIZAMISHA BIASHARA UTD MOJA KWA MOJA MPAKA LIGI YA CHAMPIONSHIP…

RASMI….AZAM FC WAIZAMISHA BIASHARA UTD MOJA KWA MOJA MPAKA LIGI YA CHAMPIONSHIP…


Biashara United ya Musoma inakuwa timu ya pili kushuka daraja msimu huu baada ya kichapo cha mabao 4-1, dhidi ya Azam FC.

Mabao ya Azam yalifungwa na Idrisa Mbombo aliyeweka kambani mabao matatu na Never Tigere dakika 79.

Mbombo alifunga mabao matatu kwenye dakika 14, 46 na 59 na kuingia katika orodha ya wachezaji watatu walioweka rekodi ya kufunga hat-trick msimu huu akimaliza msimu na mabao 9 ya Ligi kwenye mechi 17.

Hat-trick ya kwanza ilifungwa na Jeremia Juma wa Tanzania Prisons kwenye mchezo dhidi ya Namungo na nyingine alifunga Shiza Kichuya wa Namungo katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kutokana na matokeo hayo Azam imemaliza kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara iliyohitimishwa jioni ya leo Juni 29, wakati Biashara imeshuka moja kwa moja ikiwa na pointi zao 28.

Biashara inakwenda kucheza Championship msimu ujao sambamba na wenzao Mbeya Kwanza waliyotangulia mapema huko.

Matokeo mengine Mtibwa Sugar iliyofungwa na Yanga bao 1-0, na Tanzania Prison aliyofungwa bao 1-0, zitakwenda kucheza mechi mbili za playoff nyumbani na ugenini.

SOMA NA HII  BADO LA KIDEONI ALILOFUNGA SAKHO LAPETA AFRIKA...CAF WALITAJA KWENYE MABAO BORA YA MSIMU...