Home Habari za michezo CHAMA ‘AKOPOLEWA MAWE’ NA SHABIKI WA SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

CHAMA ‘AKOPOLEWA MAWE’ NA SHABIKI WA SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Clatous Chama kwa sasa hana msaada tena kwenye kikosi chao hivyo anapaswa awaachie nafasi wachezaji wengine.

Mchombe amesema baada ya siku za hivi karibuni Chama kutofanya vizuri kwenye kikosi hicho na kupelekea kupigwa benchi kwenye mechi ya ASEC Mimosas na ile ya Jwaneng Galaxy.

“Ni uongozi ndio walipanga Chama aanzie benchi kwa sababu hakukuwa na kocha kwa hiyo viongozi ndiyo walipanga timu. Lakini uhalisia ni kwamba Simba tuna hali mbaya, aliyeingia na aliyetoka hakuna mwenye uafadhali, wachezaji wote wamechoka.

“Ikifika wakati wa usajili Chama anavalishwa jezi ya Yanga viongozi wanaogopa na kumwongezea mkataba. Chama hana msaada kwa sasa kwenye kikosi, amekuwa mzigo Simba. Chama akiingia ndio mpira unakufa kabisa.

“Timu sasa hivi inabebwa na Kibu Denis, akitoka tu timu inakufa. Fitness ya Kibu iko juu kuliko wengine, je yeye ana mwalimu wake wa mazoezi? Kwa hiyo tatizo sio fitness ni wachezaji hawajitumi, wanaona wameshapata kila kitu waachane nao. Watafute wachezaji wenye uchu na mafanikio.

“Ukiangalia Yanga wachezaji wanaowika sio wale wenye mafanikio makubwa ni wale wenye uchu na mafanikio, ukiwaangali Maxi, pacome, yao Yao, Aziz Ki, lakini ukimwangalia Chama ana medali ngapi, vikombe vingapi vya ligi? Tshabalala juzi amecheza dabi ya kariakoo ya 25, bado unaye kwenye kikosi wa nini?,” amesema

SOMA NA HII  ILE SAPRIAZI YA YANGA KUMBE NI HII HAPA MASHINE MPYA YA KAZI...MWENDO 'MPERA MPERA' TU...