Home Habari za michezo UBOSI WA HERSI CAF ULIVYOIPELEKA TZ KARIBU NA MEZA YA SOKA DUNIANI…ATAFIKA...

UBOSI WA HERSI CAF ULIVYOIPELEKA TZ KARIBU NA MEZA YA SOKA DUNIANI…ATAFIKA HADI FIFA…

Habari za Yanga

Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Vilabu Africa (ACA) wakati wa uzinduzi wa shirikisho hilo.

Majukumu Mwenyekiti wa Shirikisho la vilabu vya soka Barani Afrika, Eng. Hersi Said moja kwa moja amekuwa mjumbe wa kamati tendaji ya shirikisho la soka Afrika (CAF).

Kuanzia sasa Eng. Hersi Said atakuwa anashiriki mikutano yote muhimu ya maamuzi ya (CAF), anaingia kwenye EXCOM.

Ndiye muwakilishi wa vilabu vyote Barani Africa katika Shirikisho la soka Duniani (FIFA) na Shirikisho la soka Afrika (CAF).

Kupitia uenyekiti wa Eng. Hersi Said Tanzania imepata wajumbe wawili ambao watakuwa wanapiga kura kuamua masuala mbalimbali ya uendeshaji wa soka Barani Africa kwenye mkutano mkuu wa (CAF).

Tanzania sasa inaanza kuzisogelea nafasi za juu za maamuzi ndani ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

◉ Rais wa (CECAFA) – Wallace Karia ◉ Mwenyekiti wa (ACA) – Hersi Said.

Hersi atasaidiwa na Jessica Motaung kutoka Kaizer Chiefs (South Africa) na Paul Bassey kutoka Akwa United ya Nigeria.

Full Board: African Club Association

UNAF Zone: Khaled Abdelkader (Al Ahly, Egypt) Taha Diay (Raja, Morocco)

WAFU A: Rodney Edmond Michael (Mighty Blackpool FC, Sierra Leone) Famakan Dembele (AS Real Bamako, Mali)

WAFU B Ayibatin Wilfrido (AS Loto FC, Benin) Paul Bassey (Akwa United, Nigeria)

CECAFA: Hersi A. Said (Young Africans, Tanzania) Hassan Ali Eissa (Al Hilal, Sudan)

COSAFA: Jessica Motaung (Kaizer Chiefs, South Africa) Salamo Newboy Hei (African Stars, Namibia)

UNIFFAC Ravel Mondjo Mbouloungou (CS de Bendje, Gabon) Guy Kapya Kilongozi (AS Maniema Union, DR Congo)

SOMA NA HII  MASAU BWIRE AIBUA UPYA SAKATA LA KIFO CHA SONSO...PABLO ATULIZA MZUKA SIMBA...SAIDO, AUCHO KUKIONA...