Home Habari za michezo GAMONDI AWAPANIA WAGHANA….MASTAA WOTE YANGA KUPIGISWA TIZI LA KIJESHI….

GAMONDI AWAPANIA WAGHANA….MASTAA WOTE YANGA KUPIGISWA TIZI LA KIJESHI….

Habari za Yanga

KATIKA kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna alama tatu muhimi ugenini, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewaongezea dozi ya mazoezi wachezaji wake kwa kufanya mara mbili kwa siku baada ya kikosi cha timu hiyo kuwasili salama katika mji wa Kumasi nchini Ghana.

Yanga wamewasili salama nchini humu na kuendelea na maandalizi ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama ambao utachezwa Ijumaa hii, nchini humo.

Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison amesema hakuna kulala baada ya kuwasili kwenye mji huo wa Kumasi, kocha aliwataka wachezaji kuendelea na programu ya mazoezi na jioni kupasha misulu.

Amesema program yao itakuwa ni mazoezi mara mbili kwa siku, maandalizi ambayo ni tofautina michezo iliyopita ambayo walikuwa wakifanya mara mmoja, kuelekea mchezo huo wanafanya mara mbili asubuhi na jioni.

β€œJuzi tulifika salama hatukupata changamoto yoyote, licha ya kuwa na safari ndefu na uchovu wa wachezaji haijatuzuia kutofanya mazoezi siku ile, kwa ajili ya kuwaweka sawa vijana , kesho (leo) tutakuwa na programu ya mazoezi mara mbili asubuhi na jioni uwanjani.

Hali ya hewa ni nzuri na kufika hapa mapema kwa sababu ya kuwafanya wachezaji kuzoea hali ya hewa lakini pia kupata muda wa wachezaji kuzoea mazingira ya uwanja ambao kesho (leo) tutaenda kufanya mazoezi katika dimba ambalo tutatumia katika mchezo,” amesema Walter.

Aliongeza kuwa kuwa kocha anakuwa makini na safu ya ulinzi na ushambuliaji kuhakikisha hawaruhusu bao lakini pia wanakuwa watulivu kutumia nafasi zinazopatikana ili kusaka ushindi.

Amesisitiza kuwa malengo yao makubwa ni kutafuta ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya mipango yao ya kwenda kucheza robo fainali ya mashindano hayo, ambapo kufika huku lazima washinde mechi zilizosalia.

β€œTunafahamu haitakuwa mechi rahisi kwa kuwa kocha Gamondi anaendelea kufanyia kazi mapungufu ya kikosi tuliyofanya mechi zilizopita ikiwemo kuhimiza suala la utulivu kwa washambuliaji wetu na mabeki kuwa makini kwa sababu ya ubora wa Medeama kila mechi wamefanikiwa kufunga,” amesema Meneja huyo wa timu.

Wakati huo huo, Daktari wa Yanga, Mosses Etutu amesema wachezaji waliokuwepo Ghana wako vizuri na kuendelea na majukumu yao licha ya jana kiungo Jonas Mkude alipata shida baada ya kula chakula kikamleta madhara na sasa yuko vizuri.

Kuhusu hali ya beki wao, Joyce Lomalisa, amesema nyota huyo amefanyiwa vipimo na kuonekana amepata jeraha dogo na atakuwa nje ya uwanja wa muda wa siku sana kwa ajili ya matibabu na kurejea katika majukumu yake ya uwanjani.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI