Home Habari za Yanga GAMONDI AMWAGA CHECHE…USHINDI WA 5-0 BADO HAUJAISHA…AFUNFUKA HAYA

GAMONDI AMWAGA CHECHE…USHINDI WA 5-0 BADO HAUJAISHA…AFUNFUKA HAYA

Habari za Yanga leo

YANGA imerudi njia ya ushindi baada ya kuichapa Coastal Union kwa bao 1-0 ikiendelea kupunguza safari ya kulifuata taji la 30 la Ligi Kuu Bara, lakini kocha wa Wananchi, Miguel Gamondi akafunguka namna timu hiyo ya Tanga ilivyonusurika kupigwa nyingi akimtaja kipa wa Wagosi wa Kaya, Ley Matampi.

Kocha huyo pia alifichua kwamba si kweli kwamba ushindi wa 5-0 waliokuwa wakipata umeisha, ila alisema kikosi hicho kinashuka uwanjani kusaka matokeo mazuri, ili timu
inayokaa vibaya ndio igongwe nyingi na kwamba hata juzi kama sio Matampi, Wagosi walikuwa wanakula zaidi ya mabao matano.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi alisema hakuna siku ambayo timu yake imeingia uwanjani na hesabu za kufunga mabao matano kama ilivyoshinda kwenye baadhi ya mechi za michuano iliyopo timu hiyo, lakini akasema ubora wa wapinzani ndio msingi wa wao wa kupata ushindi wa idadi kubwa ya mabao.

Gamondi alisema licha ya Coastal kucheza timu nzima nyuma ya mpira ikicheza mfumo wa kupaki basi, bado Yanga ilikuwa na nafasi ya kushinda kwa mabao mengi kama isingekuwa kipa mkongwe kutoka DR Congo,

Matampi kusimama imara langoni na kuwanyima nafasi ya kutoka na kapu la mabao. Kocha huyo raia wa Argentina, alisema Matampi alikuwa na dakika 90 bora kwa kuipunguzia Coastal idadi ya mabao kwa namna alivyocheza kijasiri kwa kuokoa mashambulizi ya Yanga ambayo kama angedaka kipa wa kiwango cha kawaida kungekuwa na habari nyingine kwa sasa katika mchezo huo uliopigwa Azam Complex.

β€œHatujawahi kutoka kambini tukasema tunakwenda
kuwafunga wapinzani mabao matano, kushinda mabao mengi inategemea na makosa gani mpinzani ameyafanya dhidi yetu, tuna staili ya soka letu namna ya kutafuta ushindi, kitu muhimu kwetu ni kushinda kwa kupata pointi tatu na kucheza soka la kuvutia,” alisema Gamondi na kuongeza; “Angalia mechi ya jana (juzi) ingewezekana kushinda mabao mengi, wapinzani wetu walijua wanakuja kukutana na timu gani wakaamua wote kucheza nyuma ya mpira bado haikuwa shida tulitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi zakufunga.

“Bahati yao (Coastal) ni kwamba langoni walikuwa na kipa mzuri ambaye sio vibaya tukimpongeza kwa kufanya kazi kubwa, kinyume cha hapo tungeweza pia kutengeneza ushindi mkubwa, kitu muhimu malengo yetu ni kushinda na tumefanikiwa.”

Matampi mwenye clean sheet 10 katika mchezo huo wa juzi dhidi ya Yanga alifanya kazi nzuri na bora akiokoa jumla ya mashambulizi tisa ambapo kati ya hayo saba ni yale ya hatari, huku mashuti 10 yalilenga lango ya Coastal. Bao la Yanga katika pambano hilo liliwekwa kimiani na Joseph Guede katika dakika ya 77, likiwa ni la nne kwake kwenye ligi hiyo iliyopo ukingoni.

Aidha, Gamondi alisema kikosi chake sasa kina ubora mkubwa ambapo wana mbinu za kushambulia kutokea pembeni, kupiga mashuti na hata kushambulia ndani ya boksi wakijua kwamba watakutana na timu zinazopaki basi.

Yanga imegawa dozi ya 5G kwa timu za JKT Tanzania, KMC, Ihefu na Simba ndani ya Ligi Kuu, ikaichapa pia Jamhuri ya Pemba katika Kombe la Mapinduzi 2024 na kuzinyoa Polisi Tanzania na Hausung zilipokutana Kombe la Shirikisho za msimu huu pamoja na kuitandika pia Asas ya Djibouti katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  NABI AIWAHI YANGA ...AAGANA NA MASHABIKI...ASISITIZA KILA KITU KITAISHA TUNISIA...