Home news NABI:- YANGA KUNA PRESHA SANA….AFUNGUKA NAMNA ANAVYOPITIA MAGUMU…AGUSIA ISHU YA UBINGWA..

NABI:- YANGA KUNA PRESHA SANA….AFUNGUKA NAMNA ANAVYOPITIA MAGUMU…AGUSIA ISHU YA UBINGWA..


NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuna presha kubwa katika kusaka ushindi uwanjani ambao utawapa ubingwa kutokana na kila timu kupiga hesabu za kuifunga Yanga.

Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 36 kibindoni baada ya kucheza mechi 14, ndani ya ligi hiyo hawajapoteza mchezo msimu huu, huku Jumatano ijayo wakitarajiwa kupambana na Ruvu Shooting.

Akizungumza na Soka la Bongo, Nabi alisema: “Presha inakuwa kubwa hasa timu inaposaka ushindi, ukizingatia kwamba ili uwe bingwa ni lazima ushinde mechi zako, hivyo hakuna tatizo katika hilo, tunalifanyia kazi.

“Kwa timu ambazo tunakutana nazo ninaona kwamba zinataka kuifunga Yanga, hapo inafanya kila mechi kwetu kuwa ngumu. Lakini inatakiwa kuwa hivyo kwa kuwa unapokuwa unashindana na mpinzani lazima awe ana malengo ya kushinda kama ambavyo sisi tunahitaji kushinda.”

SOMA NA HII  KAMA ULIKUWA HUJUI....HUYU HAPA NDIO TEPSIE ANAYEMPA NABI MAWAZO ...KAANZA KUSUMBUA WATU MAPEMA SANA...