Home Habari za michezo AHMED ALLY:- SIMBA HAKUNA UBOVU HUO KIVIILEE …AL AHLY WALITUWAHI TU….

AHMED ALLY:- SIMBA HAKUNA UBOVU HUO KIVIILEE …AL AHLY WALITUWAHI TU….

Habari za Simba SC

BAADA ya kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa misimu mitano , Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ameweka wazi kuna kazi ya ziada inabidi kufanyika, ikiwemo kupata mastraika wenye uwezo mkubwa wa kutumia nafasi zinazopatikana.

Benchikha amesema pia kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Al Ahly uliongeza ugumu kwenye mechi ya marudiano, lakini akidaikuna mambo wamejifunza na kuahidi kufanya kazi kwa msimu ujao kuwa bora zaidi.

Simba imerejea nchini akitokea Misri baada ya kutolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, kwa jumla ya mabao 3-0 katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini.

Amesema Al Ahly ni timu bora na ina wachezaji wenye uzoefu ambao wanaweza kubadili mchezo muda wowote na hilo ndilo lililowagharimu, ikiwemo kupoteza nafasi nyingi kwenye mechi ya kwanza nchini.

“Lakini hatukuzitumia na wenzetu walipata moja pekee na wameitumia hiyo hiyo, ninaimani msimu ujao tukishiriki michuano hii tutakuwa bora zaidi kwa kuwa tutakuwa tumejifunza mengi, ikiwemo kuongeza baadhi ya wachezaji wenye uzoefu ambao wanaongeza nguvu na waliokuwepo.

Nafikiri tulipopoteza mechi ya kwanza nyumbani ndipo tulipoongeza ugumu wa mechi ya marudiano, Al Ahly ni timu bora na ina wachezaji wenye uzoefu wa michuano hii,Tumejifunza na naamini tutakuwa bora katika michuano hii mwakani kama tukipata nafasi ya kushiriki,” amesema Benchikha.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally, amesema hawajilaumu kwa kutolewa na Al Ahly katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika bali wamejifunza ili wakati mwingine washiriki wakiwa bora zaidi.

Amesema hawana ubovu huo ambao unaotwajwa kwa sababu timu imeweza kufikia hatua ya robo fainali ambayo imezoeleka na sasa wanaenda kutengeneza utamaduni wa kucheza nusu fainali.

“Hakuna ubovu huo unaoimbwa, sasa tunaenda kutengeneza timu, nusu fainali sio rahisi , lazima tupambane na kuwekeza kwa kupata watu wa kutupeleka huko.

Tupo katika mchakato huu wa kuwekeza kwa kuleta watu wenye uzoefu wa kucheza nusu fainali kuja kuungana na waliopo sasa kupigania timu kufika hatua hiyo ambayo wanasimba wanaiota,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa wanafanya kazi kubwa kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye michezo yote miwili na kujiandaa kwa msimu ujao.

“Al Ahly, Mabingwa watetezi wa michuano hii, ndio timu ya Karne ya Afrika na pia kinara wa kuchukua mara nyingi taji hili kwahiyo kutolewa nao sio jambo la kusema tutakaa na kuanza kujilaumu,” amesema Meneja huyo.

Ameeleza kuwa katika miaka sita wameingia mara tano robo fainali na timu zote walicheza dhidi yao zimepotea lakini Simba imeendelea kubaki pale pale na sasa muda umefika wa kusonga mbele.

“Tulianza kucheza na TP Mazembe wakapoteza mpaka sasa ndio wanarejea, tukacheza na Kaizer Chiefs wao wamepoteza, ikaja Orlando Pirates na wamepoteza na msimu uliopita Wydad Casablanca nao wameishia hatua ya makundi lakini Simba iko vile vile kwahiyo sio jambo jepesi,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa baada ya kurejea nyumbani tunaelekeza nguvu katika michuano ya Ligi pamoja na CRDB Bank Federation Cup, dhidi ya Mashujaa FC watakaocheza ugenini, Kigoma utakaochezwa leo.

SOMA NA HII  KAMA UTANI ILA NDIO IVO ZIDANE WA BONGO KATEMWA HUKO