Home news PAMOJA JANA KUIOKOA SIMBA…MATOLA AIBUKA NA HILI KUHUSU CHAMA…ADAI UWEZO WAKE BADO...

PAMOJA JANA KUIOKOA SIMBA…MATOLA AIBUKA NA HILI KUHUSU CHAMA…ADAI UWEZO WAKE BADO SANA…


KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amefunguka kuwa bado kiungo wao mshambuliaji, Clatous Chama anahitaji michezo mingine mitatu ambayo ni sawa na dakika 270 ili kuwa timamu tofauti na sasa.

Chama tangu amerejea ndani ya timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu, amefanikiwa kucheza michezo minne ya ligi kuu dhidi Mtibwa Sugar, Kagera Sugar ,Prison na Mbeya Kwanza, huku akiwa amefunga bao moja .

Kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Dar City, Chama alifanikiwa kufunga bao moja na kutoa asisti mbili wakati Simba ikishinda 6-0.

Akizungumza na Soka la Bongo, Matola alisema: “Watu wanatakiwa kufahamu kuwa Chama anahitaji michezo mingi zaidi ya mitatu ya kucheza ili kuwa bora zaidi.

“Mchezaji anahitaji kupata michezo mingi zaidi kuonesha ubora, hivyo hata kwa Chama ipo hivyo, anahitaji muda kidogo tu atakuwa bora zaidi.”

SOMA NA HII  MAYELE AWAFUTA MACHOZI YANGA, WACHEZAJI WOTE MACHO KIMATAIFA, LIGI KUU