Home news KISA DJUMA…NABI AKIRI KUPATWA ‘KIZUNGUZUNGU’ YANGA…AFUNGUKA NAMNA ANAVYOWEWESEKA NAYE…

KISA DJUMA…NABI AKIRI KUPATWA ‘KIZUNGUZUNGU’ YANGA…AFUNGUKA NAMNA ANAVYOWEWESEKA NAYE…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameweka wazi kuwa, kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza akiwemo beki Mkongomani, Djuma Shabani, ni miongoni mwa vitu vinavyowapa changamoto kubwa ya kutimiza malengo yao.

Djuma anaendelea kukosekana kwenye michezo ya Yanga kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania. Mpaka sasa amekosa mechi mbili.

Yanga ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 35 walizokusanya kwenye michezo 13, juzi Jumamosi walishuka uwanjani kuvaana na Mbeya City katika mwendelezo wa ligi hiyo.

Akizungumzia na Soka la Bongo, Kocha Nabi alisema: “Ni kweli kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wetu ambao wanatumikia adhabu na wenye majeraha ni miongoni mwa mambo ambayo kwa kiasi fulani yanatupa wakati mgumu kwa kuwa upo utofauti kati ya mchezaji mmoja na mwingine.

“Lakini licha ya changamoto hizo, kama kikosi hatuwezi kulalamikia hali hiyo, bali tunalazimika kutumia wachezaji waliopo kupata matokeo mazuri.” Mbali na Djuma ambaye anatumikia adhabu hiyo, nyota wengine wa kikosi hicho ni majeruhi akiwemo Kibwana Shomary, Yacouba Songne na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

SOMA NA HII  LEO NI USIKU WA UEFA...KWA MTONYO KIDOGO TU ODDS ZA MERIDIANBET ZINAKUPA UHAKIKA WA MAISHA...