Home news PAMOJA NA USHINDI DHIDI YA MTIBWA…MWAKALEBELA ASHINDWA KUJIZUIA YANGA..AANIKA HALI ILIVYO NDANI…

PAMOJA NA USHINDI DHIDI YA MTIBWA…MWAKALEBELA ASHINDWA KUJIZUIA YANGA..AANIKA HALI ILIVYO NDANI…


WAKATI Yanga SC jana Jumatano ikimaliza mechi za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ikiwa kileleni, uongozi wa timu hiyo umetamba kuendelea na kasi yao waliyoianza msimu huu ili kuhakikisha wanabeba ubingwa.

Kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar, Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Mtunisia, Nasreddine Nabi, ilikuwa timu pekee kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu kati ya 16 ambayo haijapoteza mchezo baada ya kucheza mechi 14, ikishinda 11 na sare tatu, ikikusanya alama 36.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa lengo la kuchukua ubingwa wa ligi ni kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ambalo lazima lifanikiwe kutokana na mikakati waliyoipanga.

Mwakalebela alisema kuwa kabla ya kuanza kwa ligi, walikaa kikao na wachezaji, benchi la ufundi na lengo lilikuwa ni kutotoka kileleni hadi mwisho wa msimu mara baada ya kukaa hapo juu.

“Katika kila msimu, mzunguko wa pili unakuwa mgumu tofauti na wa kwanza, kwani zinakuwepo timu ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja zinazopambania kubaki katika ligi, hivyo zinacheza kwa kupania.

“Hivyo katika kupunguza presha ya ubingwa wa ligi tumewataka wachezaji wetu kuendelea na kasi waliyoanza nayo hadi mwishoni mwa msimu.

“Lengo ni kuendelea kukaa kileleni hadi mwishoni mwa msimu wa ligi, kwani tukipoteza mchezo mmoja tunapunguza gepu la pointi kwa wapinzani wetu wanaotufukuzia kwa ukaribu, tunatakiwa kushinda ili gepu la pointi liwe kubwa,” alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA KUMSAJILI MAYELE....AHMED ALLY KAIBUKA NA JIPYA HILI...AGUSIA KUSEPA KWA BALEKE..