Home Uncategorized AZAM FC YASHANGAZWA NA MATOKEO MABOVU NDANI YA LIGI

AZAM FC YASHANGAZWA NA MATOKEO MABOVU NDANI YA LIGI


 VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa wanashangazwa na matokeo mabovu ambayo wanayapata ndani ya uwanja jambo linalowafanya watafute mbinu ya kurejea kwenye ubora wao.

 Kwenye mchakato wa kusaka pointi sita kanda ya ziwa imevuna pointi mbili, ilifungwa bao moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United ya Mara na kulazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bahati amesema kuwa wamekuwa wakipambana ndani ya uwanja kusaka pointi jambo ambalo limewashangaza kushindwa kupata pointi tatu.

“Ni matokeo mabaya kwetu hasa ukizingatia kwamba tunacheza vizuri na kuwa makini katika kusaka pointi tatu, kwa sasa tumeona kwamba ni lazima tujipange upya kurejea kwenye ubora wetu.

“Safari kwenye ligi bado ndefu nasi hatujakata tamaa makosa ambayo tumeyafanya tutayafanyia kazi ili kuwa bora zaidi ndani ya uwanja,” amesema Bahati.


Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 14 za Ligi Kuu Bara, kinara ni Yanga mwenye jumla ya pointi 34 kibindoni.


Ilianza kwa kasi kwa msimu wa 2020/21 ambapo ilweza kuweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi saba bila kupoteza na kujikusanyia pointi 21.


Kocha Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi Novemba 26 alitwaa tuzo ya kocha bora mwezi Septemba kutokana na kuwa na mwendo mzuri kwa mwezi huo ila mambo yalipokuwa magumu Novemba mabosi walimfuta kazi jumlajumla.


Kwa sasa mikoba yake ipo mikononi mwa George Lwandamima ambaye amesaini dili la mwaka mmoja.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA YAMKUTA HUKO, AKWAMA KUTUA BONGO MARA MBILI