Home Uncategorized NGORONGORO HEROES KUANZA MAZOEZI YA UWANJANI LEO SAUDI ARABIA

NGORONGORO HEROES KUANZA MAZOEZI YA UWANJANI LEO SAUDI ARABIA


 KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes kimeweka kambi Riyah nchini Saudi Arabia kwa ajili ya maandalizi ya Afcon.


Chini ya Kocha Mkuu, Jamhuri Kihwelo, ‘Julio’ leo kinatarajiwa kuanza mazoezi rasmi uwanjani ikiwa piwa ni kujweka sawa kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki ambazo wanatarajia kucheza.


Mchezo wa kwanza watacheza wenyeji Saudi Arabia Desemba 11.

Kiliwasili nchini Saudi Arabia Desemba 7 na kilikuwa kikifanya mazoezi ya gym kwa sababu walipaswa kuwekwa ndani, ‘karantini’ kwa muda wa siku mbili kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.


Timu hiyo ilipata nafasi ya kufuzu kushiriki Afcon baada ya kutinga hatua ya fainali kwenye mashindano ya Cecafa baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Sudan Kusini, Uwanja wa Black Rhino, Arusha.


Ilikwama kutwaa ubingwa baada ya kunyooshwa mabao 4-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa fainali na kuwafanya wawe washindi wa pili.


SOMA NA HII  KOCHA MBELGIJI AWACHARUKIA WACHEZAJI WAKE NAMNA HII