Home news WAKATI AKIJUA TAYARI KASHAPONA..YANGA WAMPIGA STOP YACOUBA…APEWA SIKU 45…

WAKATI AKIJUA TAYARI KASHAPONA..YANGA WAMPIGA STOP YACOUBA…APEWA SIKU 45…


DAKTARI wa viungo wa Yanga, Mtunisia, Youssef Ammar, amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne, amepata nafuu na atarejea uwanjani baada ya takribani siku 45.

Yacouba yupo nje ya uwanja tangu Novemba mwaka jana alipoumia goti ambapo tayari amepatiwa matibabu nchini Tunisia.

Akizungumza na gazeti la  Spoti Xtra, Ammar alisema Yacouba ameanza program ya mazoezi ya kukimbia mbio fupi na ndefu kwa ajili ya kujiweka sawa, ikiwa ni baada ya kumaliza program ya gym.

Aliongeza kuwa nyota huyo atakuwa fiti na kamili kuanza kuipambania timu hiyo, baada ya mwezi mmoja na nusu ambao ni sawa na siku 45.

“Licha ya Yacouba kupata nafuu pamoja  na kuanza program ya mazoezi ya kukimbia mbio fupi na ndefu, lakini bado anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wangu. “Kwani bado hajapona vizuri, hivyo yupo chini ya uangalizi kwa hofu ya kujitonesha ili asirejee tena katika majeraha hayo ya goti.

“Kutokana na maendeleo yake hivi sasa, upo uwezekano wa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja na nusu,” alisema Ammar.

SOMA NA HII  KAZE AFUNGUKA JINSI ANAVYOISAIDIA YANGA KUIBA MBINU ZA KLOPP WA LIVERPOOL...