Home news WAKATI SIMBA IKIANZA KUCHANGANYA…PABLO ALAINISHIWA KAZI BARA….YANGA PRESHA JUU…CAF YATAJWA…

WAKATI SIMBA IKIANZA KUCHANGANYA…PABLO ALAINISHIWA KAZI BARA….YANGA PRESHA JUU…CAF YATAJWA…


SIMBA juzi ilimalizana nan Asec Mimosas ya Ivory Coast katika mechi ya kwanza ya Kundi D ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kabla ya kurudi uwanjani  kucheza na Ruvu Shooting, huku kocha Pablo Franco akilainishiwa Bara.

Simba itavaana na Ruvu leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya kutimka kwenda Niger kucheza mchezo wao wa pili wa michuano ya CAF dhidi ya wenyeji wao, US Gendermarin kisha kuifuata RS Berkane ya Morocco.

Mechi hizo za CAF zinapigwa kati ya Februari 20-27 kisha itarudi katika Ligi Kuu Bara na ndani ya Machi na Simba itacheza michezo mitatu, huku miwili ikiwa ya nyumbani ambazo kama Pablo atakomaa nazo badi huenda akaitia presha Yanga.

Yanga ndio vinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 36 baada ya mechi 14 ikisubiri kukamilisha duru la kwanza wiki ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya kuanza mechi za duru la pili Februari 27 kwa kuivaa Kagera Sugar jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Yanga imekuwa na presha kubwa kutokana na watani wao waliopo nyuma yao walivyozipunguza pointi kutoka 10 hadi kuwa tano, licha ya kuwa mbele kwa mchezo mmoja. Simba imeshacheza mechi 15 na ina pointi 31.

Pablo anaweza kuongeza presha zaidi kwa Yanga, kama timu yake itazitumia vizuri mechi zao mbili kati ya tatu watakazocheza ndani ya Machi kupunguza zaidi pengo la pointi, huku akiiombea Yanga ivurunde kwenye mechi zao zijazo.

Ratiba inaonyesha Simba ndani ya Machi itavaana na Biashara Utd (Mar 03), kisha itaikaribisha tena Dodoma Jiji katika mechi ya Machi 7 kabla ya kusafiri kuifuata Polisi baadaye Machi 27 mara itakapomaliza majukumu yake ya kimataifa. Kama itashinda zote itavuna pointi tisa.

Ratiba ya Yanga inaonyesha ndani ya Machi itacheza mechi mbili tu moja ya ugenini dhidi ya Geita Gold siku ya Machi 6 kisha Machi 16 italizana na KMC jijini Dar es Salaam. Hii ina maana Yanga inasaka pointi 6 ndani ya Machi, huku Azam iliyopo nafasi ya nne kwa sasa ikiwa na mechi tatu ndani ya Machi ikiwamo dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Machi 1 jijini Dar.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIKAANGA SIMBA...MBEYA CITY WAIPIGA MKWARA MZITO YANGA...

Mechi nyingine ya Azam ikiwa nyumbani ni ya Machi 05 dhidi ya Polisi kisha Machi 16 itaifuata Namungo.

Juu ya mechi hizo za Ligi zijazo, kocha Pablo alikaririwa akisema anataka ushindi ili kutimiza malengo ya klabu, huku Nasreddine alisema hataki kupoteza pointi tena baada ya suluhu ya Mbeya City wakati Abdihamid Moallin alisititiza hajaridhika na matokeo ya timu yake na kwamba anaendelea kunoa makali ili kuona wanaingia Tatu Bora.