Home news KISA MECHI YA SIMBA NA WAIVORY…YANGA WASHINDWA KUJIZUIA…WAIBUKA NA HILI JIPYA….

KISA MECHI YA SIMBA NA WAIVORY…YANGA WASHINDWA KUJIZUIA…WAIBUKA NA HILI JIPYA….


Klabu ya Yanga imesikitishwa na ina laani kitendo cha kufanyiwa vurugu, kupigwa na kuchaniwa jezi mashabiki wake, kilichofanywa na mashabiki wa klabu ya Simba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba SC na Asec Mimosas, Februari 13, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga inaamini katika uungwana kwenye mchezo wa soka, hivyo kitendo walichofanyiwa mashabiki wetu kinapaswa kulaaniwa na wadau wote wapenda michezo ndani na nje ya Tanzania, kwani hakiakisi dhana ya mchezo wa Soka na kwamba hakikupaswa kuelezwa kwa namna nyingine yoyote zaidi ya kukemewa na kukilaani vikali.

Katika kudumisha amani na mshikamano katika michezo, klabu ya Yanga kwanza inatoa pole kwa mashabiki wake wote waliokumbwa na kadhia hiyo, na pili kuwataka mashabiki wote wa Yanga nchi nzima kuendeleza uungwana na kupinga chuki na uhasama unaotaka kujengwa kwa makusudi baina ya mashabiki wa soka hapa nchini.

Hivyo basi, Uongozi wa klabu ya Yanga unawataka mashabiki wake wote kutolipiza kisasi kwa namna yoyote ile na badala yake kuwakaribisha mashabiki wenzao wa timu nyingine yoyote kufurahia pamoja mchezo wa soka bila bughudha yoyote, na kudumisha utamaduni wetu wa ustaarabu, kulinda amani, mali na usalama wa watu wote tunapokuwa viwanjani.

SOMA NA HII  BEKI AFUNGUKA NAMNA CHAMA ANAVYOTISHA..AELEZA MATESO ALIYOYAPATA..NABI NA YANGA YAKE LEO BILA AUCHO NA DJUMA...