Home news A-Z JINSI YANGA WALIVYOIMALIZA BIASHARA NNJE NDANI…DIARA ATOBOLEWA…SIMBA KUJIBU MAPIGO LEO…

A-Z JINSI YANGA WALIVYOIMALIZA BIASHARA NNJE NDANI…DIARA ATOBOLEWA…SIMBA KUJIBU MAPIGO LEO…


MABAO mawili ya Yanick Bangala na Fiston Mayele yameifanya Yanga kusonga katika hatua ya robo fainali katika kombe la Shirikisho Azam (ASFC).

Wakati Yanga wakishinda mchezo huo wanawasubili watani wao Simba ambao ni mabingwa watetezi wakicheza leo saa 1:00 usiku.

Bangala na Mayele waliitanguliza timu hiyo baada ya kila mmoja kufunga bao katika dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa 16 bora dhidi ya Biashara Utd.

Bangala ndiye alikuwa wa kwanza kufungua ukurasa wa mabao dakika 21 baada ya kupigwa kona na Saido Ntibazonkiza na mpira ukachezwa na kurudi kwa Ntibazonkiza ambaye alipiga krosi na kutokea piga nikupige na Bangala aliweka wavuni.

Biashara nao hawakuwa nyuma dakika 37 walipata bao baada ya Christian Zigah kupiga krosi na Collins Opare alionganisha kwa kichwa.

Kipindi cha pili timu zote zilianza wakionyesha kuhitaji bao la kuwapa nguvu zaidi kwene mchezo huo.

Biashara walifanya shambulizi la hatari baada ya kiungo wake James Mwashinga kupiga shuti kali ambalo kipa wa Yanga, Djigui aliutema na kuuwahi tena kisha aliudaka.

Yanga nao walijibu shambulizi hilo kupitia kwa Feisal Salum ambaye aliingia na mpira katikati ya uwanja na kufyatuka shuti kali lakini liliguswa na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Dakika 47 Leny Kissu alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Aucho.

Dakika 67  Biashara walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Leny Kissu na Christian Zigah huku nafasi zao zikichukuliwa na Boniphace Maganga na Atupele Green.

Yanga walionekana kutengeneza mashambulizi mengi lakini kwenye eneo la umaliziaji hawakuwa vizuri baada ya kupoteza nafasi nyingi.

Dakika 75 Mangalo wa Biashara alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Dickson Ambundo.

Dakika 80 Biashara walifanya mabadiliko ya kumtoa Deogratius Mafie na kuingia Mathew Odong huku Yanga wakimtoa Feisal Salum na kuingia Deus Kaseke.

Timu zingine zilizotinga hatua hiyo ni Geita Gold, Azam, Kagera Sugar, Coastal Union na Polisi Tanzania.

SOMA NA HII  SIMBA SC HAWATANII AISEE...BAADA YA MRENO KUCHOMOA...KOCHA MPYA HUYU HAPA...