Home news BAADA YA KUONA PIRA LA SIMBA JUZI…MASAU BWIRE AGUNA KISHA AKASEMA...

BAADA YA KUONA PIRA LA SIMBA JUZI…MASAU BWIRE AGUNA KISHA AKASEMA HILI KUHUSU MECHI YA LEO…


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire ameitahadharisha Simba SC kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, Hatua ya 16 Bora leo Jumatano (Februari 16).

Simba SC itakua mwenyeji wa mchezo huo utakaorindima Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, kuanzia saa moja jioni.

Masau Bwire amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa leo, na wamejipanga kuwashangaza wadau wa soka nchini kwa kutoa kipigo kikali dhidi ya Simba SC.

“Ruvu Shooting ni timu kubwa yenye wachezaji wenye ubora wa hali ya juu, hivyo Simba SC wajiandae kula kipigo kizuri ambacho kitawashangaza wadau wote wa soka Tanzania hii.”

“Simba SC waje kucheza mpira, wasithubutu kuja na matokeo yao mfukono, kwa sababu ni kitu ambacho kitawaletea madhara makubwa sana baada ya dakika 90.” Amesema Masau Bwire

Simba SC ndio Bingwa mtetezi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara mara mbili mfululizo, na tayari imeshajinasibu kuutaka tena ubingwa wa Michuano hiyo kwa mara ya tatu msimu huu 2021/22.

SOMA NA HII  YANGA MPOO....?...NABI ATAKA MAMBO KAMA YA SIMBA HUKO....PLUIJM APIGWA NA BUTWAA...