Home Ligi Kuu BARAZA:WACHEZAJI WANAFUATA MAELEKEZO, KUNA JAMBO LA KUFANYA

BARAZA:WACHEZAJI WANAFUATA MAELEKEZO, KUNA JAMBO LA KUFANYA

 FRANCIS Baraza,  Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wachezaji wake wanafuata maelekezo yake katika kusaka ushindi ila wanakazi ya kuboresha zaidi utendaji kazi wao.

Ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa imecheza jumla ya mechi 30 imekusanya pointi 33 ipo nafasi ya 13.

Baraza amesema kuwa ushindani katika Ligi Kuu Bara ni mkubwa hivyo wachezaji wake nao wanapaswa kuongeza juhudi.

“Wachezaji wangu katika mechi zao za hivi karibuni naona kwamba wanafuata maelekezo ila bado kuna jambo la kufanya ili kuwa bora zaidi.

“Tuna kazi ya kufanya katika kutimiza majukumu yetu na kwa hali ilivyo bado tuna jukumu la kupata ushindi katika mechi zetu hivyo tutafanyia kazi makosa ambayo yametokea,” amesema Baraza.

Mchezo wake wa mwisho Kagera Sugar ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting ilikuwa Mei 17.

SOMA NA HII  VITA YA KUSHUKA DARAJA, RATIBA KAMILI HII HAPA