Home Ligi Kuu KIBURI KILICHOWAPONZA SIMBA, KITAWAMALIZA COASTAL UNION

KIBURI KILICHOWAPONZA SIMBA, KITAWAMALIZA COASTAL UNION


IPO wazi kwamba kasi ambayo walianza nayo Mwadui FC ilikuwa inaonyesha kwamba kuna jambo ambalo litawatokea kabla ya msimu kuisha hatimaye limekamilika.


Haikuwa na mwanzo mzuri kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ukata na wachezaji walikuwa wanapitia mazingira magumu kwa kushindwa kulipwa stahiki zao kwa muda wa miezi kadhaa ila wakawa wanapambana.



Mwisho wa siku kwa sasa inakamilisha ratiba ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa itashiriki msimu ujao Ligi Daraja la Kwanza na ina mechi ambazo itacheza kwa sasa kukamilisha msimu wa 2020/21.


Weka kando Mwadui FC, tukumbushane kidogo kuhusu Simba ambao walikuwa ni wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kwa kasi ambayo walianza nayo kila mmoja aliamini kwamba wanakwenda kutimiza lengo lao la kutinga hatua ya nusu fainali.


Kosa la kwanza ikawa ni kiburi kosa la pili ikawa ni kiburi na kosa la tatu ikawa ni kiburi hapo ndipo anguko lao lilipotokea na ndoto yao kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa ikayeyuka.


Nasema hivyo kwa sababu niliongea awali kabisa kuhusu kuona anguko la Simba ikiwa watajiamini kupita kiasi. Niliwakumbusha habari za UD Songo na kuongea mambo mengi ya kufanya hasa kikubwa niliweka wazi kwamba nidhamu inahitajika.


Haikuwa rahisi kueleweka na mashabiki wengi wa Simba walicheki na mimi na kusema kwamba ninazingua na mengine kadhalika ila mwisho wa siku kila kitu kikawa wazi.


Kwa hatua ambayo wamefika msimu huu bado Simba wanastahili pongezi lakini wangekuwa na nidhamu na kuacha kiburi wakiwa wanapambana na wapinzani wao basi leo gii tungekuwa tunazungumza habari nyingne.


Ukiachana na Simba kwa sasa timu tatu zinapambana kushuka daraja na msimu ujao ziweze kushiriki Ligi Daraja la Kwanza, hili haliepukiki.


Miongoni mwa timu hizo ni pamoja na JKT Tanzania, Coastal Union,Gwambina hizi zipo kwenye ule mstari mwekundu lakini pia Mbeya City, Kagera Sugar, Ihefu, Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, Dodoma Jiji mpaka Namungo.


Zote hizi hazipo sehemu salama hivyo ikiwa watashindwa kuwa na nidhamu katika yale ambayo wanayafanya anguko kubwa kwao linakuja.

SOMA NA HII  RATIBA YA LIGI KUU KUTIBULIWA NA MVUA...GAMONDI ATOA YA MOYONI...BODI YA LIG YAFUNGUKA HAYA


Coastal Union ilikuwa kwenye mwendo mzuri ila ghafla mambo yamekuwa magumu ikiwa wataendelea kuwa na kiburi basi anguko kwao linakuja.

JKT Tanzania, bado mwendo wao ni kusuasua ni muhimu kuongeza nidhamu na kupambana kwa hali na mali kutimiza malengo yao.

Timu zote nina amini kwamba zikiweka nidhamu katika kupambana na kuachana na kiburi cha mafanikio basi watapata kile ambacho wanastahili.