News

BAADA YA SIMBA KUTUA JANA KICHOVU…BIASHARA UTD WAITISHIA ‘NYAU’ ….WADAI WATAPIGA KWENYE MSHONO…

admin March 2, 2022 12:07 pm


KIKOSI cha Biashara United kitawasili Dar es Salaam kwa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na Ruvu Shooting.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi Vivier Bahati alisema kuwa wamekuja kutafuta alama sita katika mechi hizo mbili ili kujikwamua kutoka nafasi za chini kwenye msimamo.

Hadi sasa Biashara ina pointi 15 ikishika nafasi ya 13 kwenye msimamo na inakutana na Simba yenye pointi 31 na ipo nafasi ya pili keshokutwa Alhamisi na baadaye itacheza na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya 12 kwa pointi 16.

“Tunahitaji alama tatu kwenye kila mchezo, tumekuja na wachezaji wote, na wanatambua umuhimu wa mechi hizo hivyo wapo tayari kwa kupambana,” alisema Vivier na kuongeza;

“Simba ni timu bora, tunaiheshimu lakini soka ni mchezo wa uwanjani, tunahitaji kushinda ndani ili kuongeza morali kwa wachezaji na kujikwamua huku chini tulipo.”

Biashara itaanza kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Mkapa timu ambayo mzunguko wa kwanza wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Karume walitoka suluhu.

EDO KUMWEMBE- SIMBA WALISTAHILI  KUCHAPWA NA WAMOROCCO…ADAI CHAMA ALIDANGANYA..SOKA LILIMSHINDA… MAYELE, CHAMA NA LUSAJO WAGOMBANISHWA…MMOJA KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI HUU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply