News

KISA WACHAMBUZI…KARIA AVUNJA UKIMYA…AWAPA ‘MAKAVU LIVE’ KWA KUHOJI KUHUSU WAAMUZI…

admin March 3, 2022 11:59 am


Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Wallace Karia kwenye semina iliyofanyika jana, amesema kuwa katika watu ambao hawautendei haki mpira wa Tanzania ni Wachambuzi wa mpira, wanaongea sana mpaka wanatoka nje ya mstari na kuharibu mpira.

“Kuna wanaojiita Wachambuzi, sijui uchambuzi wamesomea wapi. Kusema ukweli katika watu ambao hawautendei haki mpira wetu ni Wachambuzi, wao wanasikilizwa na watu halafu wanatoa maoni yao binafsi”.

“Mimi naona wao (wachambuzi) ndiyo wakati mwingine wanaopotosha na kuzua taharuki”.

“Wenzetu Wachambuzi au waandishi uliopo hapa (kwenye semina) mkitoka muwe mmebadilika, siyo mechi imeisha unamuuliza Kocha aliyefungwa goli tatu kwamba mwamuzi kachezesha vipi”. Amesema Rais wa TFF.

RASMI..CHELSEA KUPIGWA BEI….MMILIKI WAKE AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA SABABU…PUTIN ATAJWA… BAADA YA MASOUD DJUMA KUANZA NA SARE…DODOMA JIJI WAONA ISIWE TABU…WAIBUKA NA HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply