Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania ‘FAT’ kwa sasa Shirikisho ‘TFF’ Ismail Aden Rege ametoa ufafanuzi wa kauli aliyoitoa Jumapili (Machi 13) baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba SC dhidi ya RS Berkane.
Rage alizungumza na Waandishi wa habari na kutoa kauli ya kuiita Ligi Kuu Tanzania Bara ‘Ligi ya Mbuzi’ kauli ambayo ilipokelewa kwa jazba na baadhi ya wadau wa michezo nchini.
Mdau huyo mkubwa wa Soka La Bongo amesema huenda hakuelewe vizuri, lakini alimaanisha kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa imekua ngumu kwa Simba SC kufuatia Young Africans kuwa na kiwango bora, hivyo Simba SC inapaswa kuwekeza nguvu kubwa kimataifa.
“Ukiangalia Young Africans wanavyocheza huoni ni lini watapoteza mchezo ligi kuu, inahitajika nguvu ya ziada sana kuweza kuchukua ubingwa mbele ya Young Africans ambao wametuacha kwa points”
“Tumezoea kipindi kama hiki Young Africans akiwa juu hata kwa points lakini na sisi huwa tunakuwa na viporo vinne au vitano lakini kwa sasa wote tunamichezo sawa”
“Ndio maana nikasema Yanga tumewaachia ligi ya Mbuzi sisi tunawekeza kupambana kimataifa sikumaanisha kuidharau ligi kuu” amesema Ismail Aden Rage