Habari za michezo

BAADA YA KUONA SIMBA WAKIZIDI KUVUNJA REKODI CAF…MWAKALEBELA KAIBUKA NA HILI..AITAJA YANGA…

admin March 19, 2022 11:31 am


Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Fredrick Lameck Wilfred Lugano Mwakalebela ameibuka na kudai kikosi chao kina ubora wa kutisha katika ukanda wa Bara la Afrika msimu huu 2021/22.

Mwakalebela ambaye alikua kimya kwa muda mrefu amesema Kikosi chao kwa sasa kimekua na mwendelezo wa kipekee katika ligi za ndani za Afrika, jambo ambalo linaufariji Uongozi wao ambao ulipambana kukitengeneza.

Amesema katika ligi za ndani za nchi ya Afrika, Young Africans imekuwa sehemu ya klabu ambazo hazijapoteza mchezo wa Ligi Kuu msimu huu 2021/22, kutokana ubora na umakini waliojiwekea kwa timu yao na kwa mchezaji mmoja mmoja.

“Sio siri kwa sasa Young Africans ni timu tishio Afrika, mpaka sasa nimefatilia Ligi za nchi zote Afrika msimu huu Young Africans ndio timu pekee Haijafungwa na sasa wapinzani wanajua wakija Kukutana na sisi hawatoki, na moto utaendelea hadi tubebe ubingwa wa Ligi Kuu.” amesema Mwakalebela.

Young Africans baadae leo Jumamosi (Machi 19) itacheza mchezo wa Mzunguuko wa 18 wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 45, huku KMC FC ikiwa nafasi ya 07 kwa kufikisha alama 22.

HAWA HAPA MASTAA 5 WA YANGA WATAKAOKOSEKANA LEO..KAZE ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA… KOCHA MSOMALI WA AZAM NAYE ALA KIAPO ‘KUITOBOA TUNDU’ YANGA..ARINGA UWEPO WA CHAMAZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply