Azam FC

KOCHA MSOMALI WA AZAM NAYE ALA KIAPO ‘KUITOBOA TUNDU’ YANGA..ARINGA UWEPO WA CHAMAZI…

admin March 19, 2022 11:40 am


BAADA ya Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Namungo, Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Hamid Moallin, ameweka wazi kuwa amefurahishwa na ari na upambanaji wa mastaa wa kikosi hicho na kuapa kuwa anataka kuona wanaendeleza hilo katika kila mchezo, hususani mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.

Azam ambayo ilicheza michezo mitatu mfululizo bila matokeo ya ushindi, juzi Jumatano walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namungo, ushindi ambao umewafanya wapande hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 28 walizokusanya kwenye michezo 18.

Baada ya ushindi huo, Azam sasa wanajipanga kuvaana na Yanga ambao wanaonekana kudhamiria kushinda ubingwa msimu huu katika mchezo wao ujao wa ligi kuu, uliopangwa kuchezwa Aprili 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Kocha Moallin alisema: “Kwanza kabisa nawapongeza sana wachezaji wangu kwa namna ambavyo walipambana katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Namungo, ni wazi ulikuwa mchezo mgumu sana kwetu, nadhani tulikuwa tunakosa upambanaji wa namna hii kwenye michezo yetu iliyopita.

“Ninaitaka Azam ninayoifundisha mimi icheze kwa kiwango hiki kwa kila mchezo ulio mbele yetu hususan mchezo dhidi ya Yanga ambao najua ni mchezo mkubwa, lazima tuhakikishe tunatumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo dhidi yao.”

BAADA YA KUONA SIMBA WAKIZIDI KUVUNJA REKODI CAF…MWAKALEBELA KAIBUKA NA HILI..AITAJA YANGA… SIMBA WAIFANYIA UMAFIA ASEC…MO DEWJI ATUA KAMBINI…RAIS SAMIA AHUSISHWA KWENYE MCHAKATO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply