Habari za michezo

KAGERE, SAKHO NA KIBU DENIS WAPEWA FUPA LA KUTAFUNA BENIN….KIKOSI KAMILI CHA SIMBA HIKI HAPA…

admin March 20, 2022 3:38 pm


Medie Kagere amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa tano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigiwa Uwanja wa Generali Mathieu Karekou nchini Benin.

Kagere atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Pape Sakho, Rally Bwalya na Kibu Denis.

Jonas Mkude na Mzamiru Yassin wamepangwa katika idara ya kiungo wa ulinzi wakiwalinda mabeki kuhakikisha hawapati madhara.

Katika eneo la ulinzi Kocha Pablo Franco hajafanya mabadiliko yoyote kuanzia kwa mlinda mlango Aishi Manula walinzi wa pembeni pamoja na wale wa kati.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (17), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Kibu Denis (38)

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Erasto Nyoni (18), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Bernard Morrison (3), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Peter Banda (11).

BAADA YA KUSIKIA AZAM WAMEICHAPA NAMUNGO…NABI AWA MWEKUNDU GHAFLA…ADAI MAMBO NI MAGUMU… DAKIKA CHACHE KABLA YA MECHI…PABLO AIBUKA NA HILI SIMBA…KAPOMBE AVUNJA UKIMYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply