Habari za michezo

SAIDO NTIBAZONKIZA AVUTA ‘KICHUNA’ BURUNDI…KUHUSU HATMA YAKE NA KURUDI YANGA..ISHU IKO HIVI..

admin March 21, 2022 7:12 am


MSHAMBULIAJI wa Yanga  Mrundi Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ juzi amefunga ndoa na mpenzi wake Samatha Uwera (Samira) Bujumbura Burundi na sherehe kufayika kwenye ukumbi wa Beliane na anatarajiwa kutua nchini kabla ya mechi na Azam, April 6, Mwaka huu.

Wakati Saido akifurahia ndoa hiyo, chama lake Yanga lilikuwa uwanjani ikicheza mechi ya ligi dhidi ya KMC na kushinda 2-1 kwa bao la Andrew Vicent aliyejifunga na lile la pili likipachikwa kwa kichwa na Djuma Shaban.

Hata hivyo Saido hakuonekana uwanjani kwenye mechi mbili za Yanga zilizopita kutokana na kuuguza jeraha la mguu alilolipata kwenye mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar chama lake likishinda 3-0, huku akitupia bao la tatu la mchezo huo.

Na inafahamika kuwa Saido anaendelea vizuri na  atarejea nchini mwishoni mwa mwezi huu na moja kwa moja atajiuga na timu kuendelea kujifua kwaajili ya mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Azam inayotarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake.

Saido msimu huu amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga akihusika katika mabao 11 ya timu hiyo akifunga sita na kuasisti tano.

PAMOJA NA KUFUNGWA..TIKETI YA SIMBA CAF IPO HIVI…YANGA HATARII..INAGONGA KILA ANAYEKUJA… ‘SURE BOY’ AVUNJA UKIMYA YANGA…’ATAPIKA NYONGO’ KISA KUWEKWA BENCHI….ATOA MSIMAMO HUU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply