KIUNGO wa Yanga, Salum Abubakar โSure Boyโ amesema analichukia benchi na hayupo tayari kukaa benchi ndiyo maana ameanza kwa kasi kibarua chake akiwa ndani ya kikosi hicho, ili kuhakikisha anamshawishi kocha aendelee kumtumia kwenye kikosi cha kwanza.
Sure Boy alisema kuwa amekuja kufanya kazi na si kuleta mchezo kama wachezaji wengine ambao wanapotea baada ya kupata majina na kukiri kuwa anaamini bado ana nafasi ya kuonyesha kilicho bora.
Alisema ametua Yanga kikazi na atahakikisha anaitumia vizuri nafasi hiyo ya kucheza kikosi cha kwanza kwa kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa kama ambavyo wamekusudia.
Alisema atahakikisha anafanya kila juhudi ili aweze kuendelea kupata nafasi katika kikosi cha kwanza huku akiweka wazi kuwa nafasi anayocheza ina wachezaji wengi bora na walio na uchu wa kuitumikia timu hiyo.