Home Habari za michezo KWA HALI JINSI ILIVYO…YANGA WAKIZUBAA KIDOGO TU ..IMEKULA KWAO MAZIMA…ISHU IKO HIVI...

KWA HALI JINSI ILIVYO…YANGA WAKIZUBAA KIDOGO TU ..IMEKULA KWAO MAZIMA…ISHU IKO HIVI ‘MWAMBA’…

Yanga ndio timu pekee haijapoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu Bara hadi sasa, ikisaka rekodi iliyowahi kuwekwa na Simba na Azam kwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo bila kupoteza, lakini wakionywa mapema wakizubaa tu itakula kwao.

Vinara hao wa ligi wamecheza mechi 18, wakishinda 15, sare tatu na kuvuna pointi 48 kileleni mwa msimamo, wakifautiwa kwa mbali na watani wao, Simba wenye pointi 37 baada ya mechi 17 wakishinda 11, sare nne na kupoteza michezo miwili.

Kwa sasa Yanga inakabiliwa na mechi mbili ngumu dhidi ya Azam itakayopigwa Aprili 6 na ile ya Kariakoo Derby dhidi ya Simba Aprili 30, hivyo kutakiwa kujipanga kwelikweli kuweka heshima yao katika ligi hiyo.

Simba ilibeba ubingwa wa 2009-2010 bila kupoteza mechi yoyote kabla ya Azam kujibu mapigo mwaka 2013-2014, huku Wanalambalamba wakishikilia rekodi ya kucheza mechi 38 bila kupoteza.

Kupitia msimamo wa ligi, beki wa zamani wa Yanga Samson Mwamanda aliwapa tahadhari mastaa wa timu hiyo kupambana kwelikweli kulinda heshima yao, lakini wakisaka rekodi za wenzao walioziweka mapema kwa kubeba ubingwa kibabe.

Licha ya Simba kupitwa pointi 11, ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja, Mwamanda haoni kama inatosha mastaa wa Yanga kujisahau na kuona wamemaliza kila kitu.

“Ni jambo la kuamua kutokufungwa, naamanisha muda huu uwe wa kujitoa zaidi, kuliko kulewa sifa zilizopo mtaani, mwisho wa msimu wakichukua ubingwa bila kufungwa utakuwa wakati sahihi kwao kutamba kila kona.” alisema.

Aliyekuwa beki wa kati wa Simba, Kasongo Athuman alipigilia msumari kuwataka mastaa wa Yanga, kujua bado ligi ni ngumu na katika mechi zilizosalia lolote linaweza kutokea.

“Huu ni mpira, bado wana kazi ngumu, binafsi naamini wachezaji wa Simba wakikomaa na wakiifunga Yanga mzunguko wa pili watabadili upepo uliopo mtaani,” alisema.

Mtazano wa kocha wa Yanga B, Said Maulid ‘SMG’ anaona timu hiyo ipo kwenye nafasi nzuri ya kunyakua taji la Ligi Kuu, ila jambo kubwa anawataka wachezaji wasikubali kufungwa.

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI KIPYA CHA YANGA MSIMU WA 2023/2024

“Natamani kuona Yanga ikichukua ubingwa bila kupoteza, hilo linawezekana kama watakomaa, kwani wapo kwenye morali inayotokana na kushinda mfululizo.”