Home Habari za michezo BAADA YA KUIONA KAZI YAKE..NABI AMPITISHA AZIZ KI…NI YULE ALIYEWAUA SIMBA BENINI…ISHU...

BAADA YA KUIONA KAZI YAKE..NABI AMPITISHA AZIZ KI…NI YULE ALIYEWAUA SIMBA BENINI…ISHU IKO HIVI…


SIMBA imetua juzi ikitokea nchini Benin ambako walipoteza kwa mabao 3-0 lakini mtu ambaye aliwafunga Wekundu hao nyumbani na ugenini watani wao Yanga wameanza hesabu kali za kumshusha msimu ujao.

ASEC Mimosas ambao sasa wanaongoza kundi D la Simba wana mshambuliaji wao mmoja hatari Stephan Aziz KI ambaye amewafunga Simba nyumbani na ugenini ndio mtu ambaye ameanza mazungumzo na Yanga.

Mshambuliaji huyo raia wa Burkina Fasso anakotokea Yacouba Sogne wa Yanga, wanataka kumuongeza kwa msimu ujao wakipiga hesabu kwamba lazima wakate tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kasi waliyonayo sasa kwenye Ligi Kuu.

Hesabu za Yanga kwa KI ambaye amefunga mabao matatu katika Kombe la Shirikisho zilianzia hapa nyumbani baada ya kocha wao Nasreddine Nabi kuona makali yake na kuwaonyesha viongozi kwamba; “Namtaka yule.”

Inafahamika kwamba Nabi ambaye leo au kesho atakwenda kwao Ubelgiji kwa mapumziko mafupi, alitaka mshambuliaji huyo aangaliwe katika mchezo wa pili ambapo tayari amesharidhika na ubora wake na baadhi ya mechi ya Simba, meneja wa Sogne alianza mazungumzo na Aziz na kumuunganisha na matajiri wa Yanga, GSM.

Nabi anamtaka KI kuja kusaidiana na Fiston Mayele katika safu yao ya ushambuliaji kwa msimu ujao. “Tunaendelea na mazungumzo naye nafikiri kila kitu kinakwenda sawa tuache tufanye kazi,”alidokeza mmoja wa viongozi wa usajili wa Yanga akidai kwamba mchezaji huyo ameonyesha mzuka sana wa kuja Tanzania.

Yanga pia imewasiliana na bosi mmoja wa ASEC wakiulizia uwezekano wa kuuziwa mshambuliaji mwingine Karim Konate lakini wakajulishwa kuwa mwisho wa msimu anauzwa nchini Uholanzi kwa pesa ndefu ambayo Yanga hawawezi kuisogelea.

Konate licha ya kuwa staa muhimu ndani ya ASEC ndiye aliyepiga penalti ya kwanza katika mchezo dhidi ya Simba lakini kipa Aishi Manula akacheza.

Wakati mabosi wakijipanga hivyo Nabi naye amempa pia kazi mshambuliaji wao, Yacouba Sogne ambaye yuko kwao kwa mapumziko kuhakikisha anaweka mazingira sawa ya KI kutua ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao, lakini amewahakikishia kwamba staa huyo anapatikana kwa gharama ya kawaida.

SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI KUMI NA MOJA AMBAO WAPO WAPO TU ...WACHEZE, WASICHEZE HAKUNA ANAYEJALI...

Kwenye dirisha dogo Yanga iliwasajili kina Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Denis Nkane, Crispin Ngushi, Abuutwalib Mshery, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ na Chico Ushindi.

Waliopigwa chini ni Ramadhan Kabwili, Ditram Nchimbi na Adeyun Saleh.

Yanga imesaliwa na mechi 12 kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu.

MIKATABA MIPYA

Mjumbe wa kamati ya usajili Yanga, Hersi Said alisema wanachokiangalia sasa ni kuhakikisha timu inatwaa taji la ubingwa na wanatambua wana wachezaji wengi hawana mikataba hilo haliwapi shida kwani walio kwenye mipango yao watawaongeza.

“Ni kweli tuna idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu na wange ni miongoni mwa chachu ya mafanikio yetu sasa,” alisema.

“Hatukurupuki kuongeza watu mikataba kama unavyoona malengo yetu sasa ni taji, hivyo kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi tunatakiwa kuwa na mastaa ambao watatubeba kwenye michuano hiyo.”

Alisema kwa sasa usajili wao utazingatia wachezaji ambao hawana majeraha ya mara kwa mara ili kuendana na kasi kama watapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.