Home Uncategorized NAMUNGO: MOTO WA LIGI KUU BARA SI MCHEZO

NAMUNGO: MOTO WA LIGI KUU BARA SI MCHEZO


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa Ligi Kuu Bara ina ushindani mkubwa jambo linalofanya kila mechi kwakwe kuwa ni zaidi ya fainali.

Namungo ikiwa Uwanja wa Majaliwa ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na Alliance na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 32 baada ya kucheza mechi 18 za Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tano.

Thiery amesema:-“Kuko na ushindani mkubwa wa ligi na kila timu inapambana kupata matokeo mazuri, hata wachezaji wangu wanalitambua hilo nawapongeza kwa juhudi ambazo wanazifanya, ni wakati wetu kuonyesha kile ambacho tunacho tutaendelea kupambana,”.

Alliance ya Mwanza inafikisha jumla ya pointi 21 ikiwa nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi 18.

SOMA NA HII  GAMONDI AWATULIZA PRESHA WACHEZAJI WA YANGA.......... MECHI NI YETU HII