Home Uncategorized KUMUONA SIBOMANA, JUMA BALINYA NI BUKU TANO TU TAIFA

KUMUONA SIBOMANA, JUMA BALINYA NI BUKU TANO TU TAIFA

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kuelekea siku ya kilele cha Mwananchi Agosti 4 mambo yamekamilika kwa asilimia kubwa ni suala la mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Kesho Jumapili uwanja wa Taifa kutakuwa na shughuli maalumu kwa Yanga kutambulisha wachezaji wapya wa tiu kwa ajili ya msimu mpya wa 2019/20 pamoja na kuzindua wimbo mpya wa Yanga.

Pia uzi mpya wa Yanga utazinduliwa kesho uwanja wa Taifa na ktakuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Kariobangi Sharks kutoa Kenya.

Kuelekea kwenye mchezo huo kuwaona akina Patrick Sibomana, Juma Balinya, Mrisho Ngassa, Ally All, Mapinduzi Balama na nyota wengine kiingilio cha kawaidia ni 50,00 (buku tan) huku Vip B ikiwa ni 30,000 na Vip A  100,000


Dismas Ten, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi na kutoa sapoti kwa timu yao.

SOMA NA HII  TAMKO LA YANGA JUU YA SUALA LA KABWILI KUPEWA IST NA SIMBA