Home Habari za michezo BAADA YA KUIZIBUA REAL MADRID 4-0..BARCA WATAKA KUFANYA KISICHOWEZEKANA MSIMU HUU…

BAADA YA KUIZIBUA REAL MADRID 4-0..BARCA WATAKA KUFANYA KISICHOWEZEKANA MSIMU HUU…


Chukua karatasi na kalamu tuanze kuhesbu kwa pamoja. Kwenye hesabu, hakuna kisichowezekana wanasema.

Na Barcelona inataka kufanya kisichowezekana, kuwezekana kwenye La Liga msimu huu.

Kabla ya usiku wa juzi Jumapili kwenye El Clasico, tofauti ya pointi baina ya Barcelona na Real Madrid zilikuwa pointi 15. Jeshi hilo la Xavi Hernandez lilikuwa kwenye nafasi ya nne katika msimamo na hakuna ambaye angeanza kufikiria hesabu za kuirudisha Barcelona kwenye ndoto za ubingwa. Dakika 90 za uwanjani Santiago Bernabeu, Los Blancos wakikubali kichapo cha mabao 4-0 nyumbani, kila kitu kimebadilika. Sasa kinafikirika kisichokuwa kikifikirika huko nyuma.

Kabla ya mchezo huo, Barca ilikuwa haijapoteza mechi yoyote kati ya 12 zilizopita. Hivyo, kile walichofanya Bernabeu kinatuma ujumbe kwamba Xavi kuna kitu anajaribu kukipima kwa wapinzani wao hao kwenye mbio za ubingwa wa La Liga. Unavyosomeka msimamo kwa sasa, Barca imecheza mechi 28, imeshinda 15, sare tisa na vichapo vinne. Imefunga mabao 56, imefungwa 29 na imevuna pointi 54. Wapinzani wao, Los Blancos wamecheza mechi 29, wameshinda 20, wametoka sare sita na kupoteza mara tatu. Wamefunga mabao 59 na kufungwa 25, huku wakiwa wamevuna pointi 66.

Namba kwa sasa zipo upande wa Carlo Ancelotti na timu yake. Lakini, kama Xavi atashinda kiporo chake, pengo la pointi litapungua na kufikia tisa. Si hesabu ngumu kwa Barca kuweza kupindua meza. Kiporo cha Barca itacheza na Rayo Vallecano.

Kwa kiwango cha Barca inachokionyesha kwa siku za karibuni si timu inayoweza kupoteza pointi nyingi katika kuelekea mwisho wa msimu. Hivyo, hatima ya Real Madrid kwenye mbio za ubingwa wa La Liga zipo kwenye mikono yao wenyewe, watavuna nini kwenye mechi zao zilizobaki. Kitu ambacho Ancelotti anapaswa kufanya kutoka sasa kuepuka kupoteza mechi tatu kati ya tisazilizobaki. Hata sare pia si kitu ambacho Los Blancos inahitaji kupata kwenye mechi zao nyingi zilizobaki.

Hata hivyo, kwa upande wa Barcelona nao hawapaswi kufanya kosa lolote. Kitu ambacho inapaswa kufanya ni kuzidi kuiweka Real Madrid kwenye presha kubwa kwa kushinda mechi zake. Xavi alituma ujumbe mahsusi huko Bernabeu kwamba kikosi chake kwa sasa kna morali kubwa na kipo tayari kwa mapambano hadi mwisho wa msimu.

SOMA NA HII  NYOTA YA MAYELE YAZIDI KUWAKA YANGA...AFANYA MAKUBWA HAYA MAPYA

Kitu kingine ambacho kinaweza kuwa faida kubwa kwa Barca ni wapinzani wao Real Madrid kuendelea kuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Miamba hiyo imefika kwenye hatua ngumu zaidi, hivyo huenda akili yao ikaelekea kwenye kushinda taji hilo kubwa la ngazi ya bara na kutengeneza upenyo kwa Barcelona kutumia fursa. Barca wapo kwenye Europa League, lakini si michuano ambayo watatumia nguvu sana kutaka kubeba ubingwa. Kwa upande wao, Europa League imekuja tu kibahati mbaya.

Sawa, pengo la pointi kwa sasa ni 12, lakini kinachoonekana kutokana na mechi zao zilizobaki, vita ya kusaka ubingwa wa La Liga inaweza kuwa tamu hadi mwisho kabisa. Timu hizo zote mbili bado hazijacheza na Sevilla na Real Betis, ratiba ngumu kabisa kwa sababu chochote kinaweza kutokea kwenye mechi hizo.

Barca imebakiza mechi na Sevilla, Levante, Cadiz, Real Sociedad, Rayo Vallecano, Mallorca, Real Betis, Celta Vigo, Getafe na Villarreal. Kwenye orodha ya mechi hizo, nyingi Barca itacheza ikiwa nyumbani Nou Camp.

Madrid wao mechi zao zilizobaki Celta Vigo, Getafe, Sevilla, Osasuna, Espanyol, Atletico Madrid, Real Betis, Cadiz na Levante. Ancelotti anashughuli pevu kwa sababu hajamalizana na mahasimu wake wa Madrid, Atletico Madrid hapo akiwa na mechi ya Sevilla na wagumu ambao mara nyingi wamekuwa wakimpa shida, Real Betis. Hiki ndicho kinachofanya La Liga kuwa na nafasi ya kuona kisichowezekana kuonekana msimu huu.