Home Uncategorized SIMBA YALIPA KISASI KWA MWADUI FC, MBISSA MIKONO MIA AKIONA KICHWA CHA...

SIMBA YALIPA KISASI KWA MWADUI FC, MBISSA MIKONO MIA AKIONA KICHWA CHA KAHATA


FRANCIS Kahata, kiungo wa Simba leo amewainua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la ushindi lililowapeleka hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 2-1.

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa kisasi kwa Simba baada ya kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na bao lilifungwa na Mdamu ambaye leo amefunga pia bao kwa Mwadui.Mwadui FC ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya 34 kupitia kwa Gerald Mdamu dakika ya 34 akimalizia pasi ya Ludovick.

Bao pekee la kuweka mzani kwa Simba lilifungwa na Clatous Chama akiwa nje ya 18 dakika ya 45+2.

Kipindi cha pili Simba walifanya mashambulizi ya kutafuta bao la ushindi sawa na Mwadui na dakika ya 84 ilijiandikia bao la pili la ushindi kupitia kwa Francis Kahata aliyemalizia pasi ya Shomari Kapombe kwa kichwa na kuwanyanyua mashabiki wa Simba.

Simba inatinga hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho na Mwadui FC inafungasha virago jumla.

SOMA NA HII  KIUNGO 'ALIYEJIFUNGA' MIAKA MINNE YANGA ANA TUZO MKONONI