Home Uncategorized SABABU YA TANZANIA PRISONS KUHAMISHIA MAKAZI YAO UWANJA WA NELSON MANDELA, RUKWA...

SABABU YA TANZANIA PRISONS KUHAMISHIA MAKAZI YAO UWANJA WA NELSON MANDELA, RUKWA HII HAPA

 

UONGOZI wa Tanzania Prisons umesema kuwa sababu kubwa ya kuhamishia makazi yao mkoani  Rukwa ni kupisha ukarabati wa hostel zao pamoja na uwanja wao wa mazoezi uliopo Mbeya.

Prisons inayonolewa na Kocha Mkuu,  Salum Mayanga ambaye alikuwa akiinoa Ruvu Shooting msimu wa 2019/20 itatumia Uwanja wa Nelson Mandela msimu huu wa 2020/21 kwa mechi zake zote.

Katibu wa Prisons, Ajabu Kifukwe amesema kuwa msimu wote watakuwa Rukwa na Uwanja wa Nelson Mandela ndio utakuwa Uwanja wa nyumbani.

“Tumeamua kuhamia Rukwa ili kupisha ukarabati wa hostel zetu pamoja na ukarabati wa uwanja wetu wa mazoezi,” amesema. 

Mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara Septemba 6 itakuwa dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  PAMBA SC WAISHUKURU TPLB NA TFF KWA MKWANJA WA MILIONI MOJA, WAJA NA OMBI JINGINE