Home news BAADA YA KUONA PIRA BIRIANI LA SIMBA…KOCHA WA DODOMA JIJI KAONA ASIWE...

BAADA YA KUONA PIRA BIRIANI LA SIMBA…KOCHA WA DODOMA JIJI KAONA ASIWE TABU…KAMWAGA MISIFA KIBAO…


Kocha Msaidizi wa Dodoma Jjji FC Mohamed Muya amewaomba radhi viongozi na mashabiki wa klabu hiyo, kufuatia kupoteza mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mabingwa watetezi Simba SC.

Muya aliyekua kwenye Benchi la ufundi kufuatia Kocha Mkuu Masoud Djuma Irambona kutokuwa na vibali vya kufanyia kazi, amesema halikua kusudio la kikosi chake kupoteza mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Machi 07).

Amesema wachezaji wake wamepambana kwa nguvu zote na kwa bahati mbaya matokeo hayakua rafiki kwao.

“Sio rahisi kukubali kupoteza mchezo, inaumiza kwa kweli, ninawaomba radhi mashabiki na viongozi kwa matokeo haya.”

“Simba SC wamecheza vizuri na wamestahili ushindi, tulijitahidi kuwabana kipindi cha kwanza tukafanikiwa, kipindi cha pili mambo yalibadilika wakapata mabao mawili yaliyotukosesha alama kwenye mchezo huu.”

Naye Beki na Nahodha wa Dodoma Jiji FC Jaffar Kibacha amesema walipambana kadri ya uwezo wao ili wapate alama kwenye uwanja wa ugenini ila mambo hayakua kama walivyotarajia.

“Tulijipanga kushinda ama kutoa sare katika Uwanja huu, lakini bahati haikuwa kwetu, tumeyakubali matokeo haya na tunajipanga kwa ajili ya michezo ijayo.” amesema Kibacha.

Mabao ya Simba SC katika mchezo huo yamepachikwa wavuni na Clatous Chama kwa mkwaju wa penati na Meddie Kagere.

Ushindi huo unaiwezesha Simba SC kufikisha alama 37 zinazoiweka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakitanguliwa na Young Africans iliyo kileleni kwa alama 45.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO WASAINI BIASHARA UNITED, BEKI PIA NDANI