Home news CHAMA AIOKOA SIMBA KUABISHWA NA WATOTO WA CAMBIASSO…MSUVA ACHEZA MWANZO MWISHO….

CHAMA AIOKOA SIMBA KUABISHWA NA WATOTO WA CAMBIASSO…MSUVA ACHEZA MWANZO MWISHO….


KLABU ya Simba imeibuka na ushindi na 2-1 kwenye mchezo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Cambiasso kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju.

Mshambuliaji Simon Msuva ni kati ya wachezaji wa Cambiasso ambao wanacheza mechi hiyo na kufanikiwa kufunga bao.

Msuva yupo nje ya timu yake ya Wydad ya Morocco, huku sababu ikitajwa na kudai maslahi yake na kukaa kwake Cambiasso ni kulinda kiwango chake.

Katika mchezo huo hadi wanaenda mapuziko ubao ulikuwa unasoma Simba 1-1 Cambiasso kwa mabao ya Simon Msuva na Erasto Nyoni.

Kipindi cha pili kiungo wa Simba, Clatous Chama alikosa penalti dakika ya 68, ambapo shuti lake liliishia mikononi mwa kipa wa Cambiasso.

Penalti hiyo, ilitokana na Bernard Morrison kuwapangua mabeki wa Cambiasso, kisha akaangushwa ndani ya 18 akiwa katika harakati ya kufunga.

Chama alifunga bao la pili dakika ya 76, ilikuwa kazi ya Yusufu Mhilu ambaye akipambana na mabeki wa Cambiasso, akitokea pembeni ya uwanja kisha kutoa pasi kwa mfungaji.

Mechi hiyo, ilichezwa dakika 78 Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1, yakifungwa na Erasto Nyoni, Clatous Chama kwa Cambiasso alifunga Simon Msuva.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- KUSHANGILIA YANGA KUPANGWA NA MAMELOD NI AIBU KWETU....