Home Uncategorized KEVIN DE BRUYNE AJIPA UBALOZI WA HIYARI

KEVIN DE BRUYNE AJIPA UBALOZI WA HIYARI


KIUNGO mtengeneza mipango ndani ya Klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne amesema kuwa amekuwa balozi mzuri kwa sasa kwenye familia yake kuhusu kujilinda na Virusi vya Corona.
Kiungo huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Ubelgji amesema kuwa mwanzo familia yake ilikuwa na hofu kubwa kuhusu maambukizi hayo jambo lililomfanya awe balozi mzuri kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona.
Nyota huyo kwa msimu wa 2019/20 ametupia jumla ya mabao nane na kutoa pasi 16 za mabao akiwa ni kinara kwa kutengeneza pasi za mwisho msimu huu.
Kwa sasa Ligi Kuu England imesimamishwa na inatarajiwa kurejea Aprili 30 huku klabu zikihitaji Ligi Kuu England imalizike Juni 30.
“Kulikuwa na hofu kwa familia yangu mwanzo jambo ambalo lilinifanya niweze kuzungumza na mke wangu pamoja na watoto kuhusu kujilinda kuwa salama na maambukizi haya ya Virusi vya Corona, ninajua kwa mashabiki pia hali yao ni ya huzuni kutokana na kupenda mpira lakini afya ni muhimu zaidi,” amesema.
SOMA NA HII  MO AJIBU MAPIGO YA GSM